Nimeshtushwa sana na kifo cha Kiongozi huyu mashuhuri
aliyechangia kwa dhati harakati za ukombozi wa Bara la Afrika.
Nimehuzunishwa mno, mimi Binafsi, Familia yangu na nina imani msiba huu
mzito sio wa Watanzania peke yao, bali ni wa Bara zima la Afrika kwa
ujumla. Katika harakati za kumzika kiongozi huyo, sitokuwepo kwa kuwa
niko safarini lakini nitawakilishwa na wanangu wakiongozwa na Dkt
Hussein. Kwa Mola tumetoka na kwake Mola sote tutarejea. Mwenyezi Mungu
ailaze roho ya Marehemu mahali pema peponi
Amin
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...