Makamu Mkuu wa Chuo cha Bagamoyo.Profesa Costa Mahalu akizungumza na waandishi wa habari leo juu ya utumiaji wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama) katika semina iliyofanyika leo katika hoteli ya New Afrika,Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Sayansi,Teknolojia na Mawasiliano,Profesa Patrick Makungu akizungumza na waandishi wa habari leo juu ya utumiaji wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama) katika semina iliyofanyika leo katika hoteli ya New Afrika,Jijini Dar es Salaam.
Meneja Mradi wa Idara ya Uchumi na Mendeleo ,Mazingira na Utalii wa Afrika Kusini,Rolda Rapotu akizungumza na  katika semina ya wadau wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano iliyofanyika  leo katika hoteli ya New Afrika ,Jijini Dar es Salaam.PICHA NA EMMANUEL MASSAKA

=========  ==========  ===========

Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.
 
Wizara ya Sayansi,Teknolojia na Mawasiliano imesema itaendelea kudhibiti matumizi ya mtandao katika kuhakikisha hayatumiki vibaya kwa watumiaji.

Hayo ameyasema leo Katibu Mkuu wa Wizara ya Sayansi,Teknolojia na Mawasiliano,Profesa Patrick Makungu wakati wa Semina ya Maendeleo ya Jamii na Utumiaji Teknolojia ya Habari na Mawasiliano iliyofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya New Africa,Jijini Dar es Salaam.
 
Makungu amesema kuwa Wizara ya Sayansi,Teknolojia na Mawasiliano imepitisha sheria ya matumizi ya mitandao katika kulinda ili kulinda matumizi hayo yasitumike vibaya na kuharibu sura ya nchi.Amesema kuwa tafiti mbalimbali za mitandao  zimeanza 2010 hali ambayo zinaendelea na kufanya hivyo itasaidia nchi kupata maendeleo katika sekta ya mawasiliano.
 
Naye Mratibu wa Semina ya Maendeleo ya Jamii na Utumiaji Teknolojia ya Habari na Mawasilino,Profesa Benson Nindi amesema kuwa wanaufanya mradi huo katika suala zima la kutoa elimu juu ya utumiaji wa mitandao na serikali ya Tanzania inatakiwa kutunga sera ambayo itasaidia wananchi kwenda kasi na teknolojia ya habari na mawasiliano.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...