Wanajeshi wa nchini Nepal wakiwa wamebeba misaada kwaajili ya wahanga wa tetemeko la ardhi
Kwa Msaada wa mtandao.
Serikali ya Nepal imejitetea dhidi ya malalamiko juu ya misaada ya
dharura, kufuatia tetemeko kubwa la ardhi lililotokea Jumamosi nchini humo.
Mkuu wa masuala ya dharura wa Nepal,Rameshwor Dangal,ameambia BBC
serikali inajitahidi iwezavyo, lakini mkasa huo ulikumba majimbo 20 nchini humo
na hivyo mahitaji ni mengi sana ndiposasa serikali inaelemewa.
Hali ya kutamauka imewakumba wengi waliothiriwa na tetemeko hilo,na
wengine wameonesha malalamiko yao kwa kulumbana na polisi huko Kathmandu, mji
mkuu wa taifa hilo.
Angalau sasa misaada ya bidhaa muhimu na huduma zimeanza kuwafikia waavijiji
katika mji wa Kathmandu nchini humo.
Wakati huo huo, Mwanamme aliyetolewa ndani ya kifusi katika hoteli
iliyoporomoka mjini Kathmandu ameelezea jinsi alivyoweza kuishi kwa saa 82
kabla ya kuokolewa.
Rishi Khanal amesema alilazimika kunywa mkojoo wake wakati akisubiri
kuokolewa.
Mguu wake alikwama ndani ya kifusi lakini aliweza kuwasiliana na jamaa
zake akitumia simu yake ya mkononi.
Hata hivyo hakumbuki hoteli alimokuwa, aliokolewa na makundi ya uokoaji kutoka
nchini humo na Ufaransa.
Zaidi ya watu 5000 wamepoteza maisha katika janga hilo la tetemeko la ardhi
huko Nepal.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...