Na Mwandishi Wetu
Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Mh.Subira Mgalu amezindua Shindano la Mama Shujaa wa Chakula linaloendeshwa na Shirika lisilo la kiserikali la Oxfam kupitia kampeni ya Grow lenye lengo la Kumuwezesha Mwanamke katika kilimo na kumkwamua kiuchumi.
Subira ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kumwezesha mwanamke katika kilimo na kumkwa mwanamke kiuchumi iliyofanyika katika kijiji cha Kisanga wilayani Kisarawe mkoani Pwani.
Subira amesema kufanyika kwa mashindano wilayani kwake ni fursa kwa wanawake kushiriki kuchukua fomu za ushiriki na kuacha uvivu na kutaka zawadi ya mshindi wa kwanza itokee wilyani humo.
Aliongeza kuwa shindano hilo linawapa mwanamke uwezo wa kutambua haki zao umiliki wa ardhi na kuwa na ubunifu wa kuweza kubadilisha mbinu za kisasa za kilimo bora.
Nae Mwakilishi kutoka Oxfam Eluka Kibona amesema kijiji cha Kisanga ndicho kitakuwa wenyeji wa shindano hivyo wanawake wa kisarawe wanahitaji kujituma katika kuchangamkia fursa hiyo.
Pia Diwani wa Kata ya Masaki Mh. Pily Chamnguhi aliwasihi akina baba wa Kisarawe kuwaruhusu wake zao na watoto wao wa kike kuchukua fomu kwa wingi na kushiriki katika shindano hilo kwa kuwa hiyo ni moja ya fursa ambazo watazipata kupitia Shindano la Mama Shujaa wa Chakula..jpg)
.jpg)
Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Mh. Subira Mgalu akizungumza na wananchi wa wilaya hiyo wakati uzinduzi wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula 2015 akizindua Rasmi Mashindano hayo katika kijiji cha Kisanga Mashindano yatakapofanyikia.
Meneja Utetezi na Ushawishi wa Oxfam,Eluka Kibona akielezea Shindano la Mama Shujaa wa Chakula.
Diwani wa Kata ya Masaki Mh. Pily Kondo Changuhi akizungumza na Wakazi wa Kisarawe pamoja na wageni waalikwa katika Sherehe hizo za uzinduzi wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula.
BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI
BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...