Meneja wa Bia ya Safari Lager, Edith Bebwa(kushoto) na Mrakibu Mwandamizi wa
Jeshi la Polisi, Gerald Ngiichi wakimkabidhi kikombe mchoma nyama mkuu
wa Bar Soccer City ya Sinza, Said Dando mara baada ya kuibuka
mabingwa katika mashindano ya Safari Lager Nyama Choma jijini Dar es
Salaam yaliyofanyika katika viwanja vya Leaders mwishoni mwa wiki.
Mrakibu Mwandamizi wa Jeshi la Polisi, Gerald Ngiichi(wa pili kushoto)
wakimkabidhi kitita cha Shilingi 1,000 ,000/= mchoma nyama mkuu wa
Bar Soccer City ya Sinza, Said Dando mara baada ya kuibuka mabingwa
katika mashindano ya Safari Lager Nyama Choma jijini Dar es Salaam
yaliyofanyika katika viwanja vya Leaders mwishoni mwa wiki.Kushoto
ni Meneja wa Bia ya Safari Lager, Edith Bebwa.
Na Mwandishi Wetu.
SOCCER City Bar yenye makazi yake Sinza jijini Dar es Salaam wameibuka
mabingwa katika fainali za mashindano ya Safari Lager Nyama Choma 2015
yaliyofanyiaka mwishoni mwa wiki katika Viwanja vya Leaders Klabu na hivyo
kuzawadiwa fedha taslimu Shilingi milioni moja na Kikombe.
Nafasi ya pili ilichukuliwa Chamanzi Bar ya Mbagala ambayo ilizawadiwa pesa
taslimu Shilingi 800,000/=,nafasi ya tatu ni Liquid Barya Chang’ombe ambayo
ilizawadiwa pesa taslimu Shilingi 600,000/=,nafasi ya nne ni High Way Bar ya Boko
ambayo ilizawadiwa Shilingi 400,000/=, nafasi ya tano ni Amaholo Bar ya Salasala
ambayo ilizawadiwa Shingi 200,000/- na nafasi ya sita ni Kilwa road Bar ambayo
ilizawadiwa pesa taslimu Shilingi 100,000/=.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...