Brigedia Jenerali Hashim Iddi Mbita (mstaafu) enzi za uhai wake.


JESHI LA ULINZI LA WANANCHI WA TANZANIA

Simu ya Upepo   : “N G O M E”             Makao Makuu ya Jeshi,
Simu ya Mdomo : DSM  22150463         Sanduku la Posta 9203,
Telex                     : 41051                          DAR ES SALAAM,  28 Aprili, 2015.
Tele Fax                : 2153426
Barua pepe       : ulinzimagazine@yahoo.co.uk
Tovuti                  : www.tpdf.mil.tz
                  
Taarifa ya kifo kwa Vyombo vya Habari
Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) linasikitika kutangaza kifo cha Brigedia Jenerali Hashim Iddi Mbita (mstaafu) kilichotokea tarehe 26 Aprili 2015, 
Brigedia Jenerali Hashim Mbita (mstaafu) alizaliwa tarehe 02 Novemba 1933 katika mtaa wa Songoro, Kata ya Gongoni, Wilaya ya Tabora Mjini, katika Mkoa wa Tabora.  Alisoma shule ya Msingi ya Government Town Primary School Mkoani Tabora kuanzia mwaka 1946 hadi 1949. Alijiunga na Government Secondary School Tabora Mwaka 1950 hadi alipohitimu kidato cha sita Mwaka 1957. Mwaka 1960 alijiunga na Chuo cha East African School of Co-operatives kilichopo Nchini Kenya.  

Marehemu Brigedia Jenerali Hashim Mbita baada ya masomo yake alijiunga na JWTZ tarehe 01 Novemba, 1968 na kutunukiwa Kamisheni tarehe 26 Aprili, 1969.  Alistaafu Utumishi Jeshini kwa Heshima tarehe 31 Desemba 1992.
Katika utumishi wake marehemu alishika Madaraka mbalimbali Ikiwemo Mkaguzi msaidizi Mkoa wa Mwanza mwaka 1958 hadi 1960, Afisa Habari Mkoa wa Dar es Salaam mwaka 1960 hadi 1962, Afisa Habari Mkuu wa Serikali mwaka 1962 hadi 1965, Mwandishi wa Habari wa Rais mwaka 1965 hadi 1967, Katibu mwenezi wa TANU Mkoa wa    Dar es Salaam mwaka 1967 hadi 1968,

Mwalimu wa Siasa Chuo cha Maafisa Monduli 1969 hadi 1970, Katibu Mtendaji wa OAU Kamati ya Ukombozi mwaka 1972 hadi 1989 na Balozi wa Tanzania Nchini Zimbabwe mwaka 2003 hadi 2006.

Marehemu Brigedia Hashim Mbita ameacha mke na watoto.  Mwili wa marehemu unatarajiwa kuagwa rasmi tarehe 29 Aprili, 2015 kuanzia saa 1:30 hadi 5:00 asubuhi katika Hospitali Kuu ya Jeshi Lugalo na mazishi yatafanyika katika makaburi ya Kisutu Jijini Dar es Salaam, saa 10:00 jioini baada ya Sala ya adhuhuri.

MUNGU AILAZE MAHALI PEMA PEPONI ROHO YA MAREHEMU
BRIGEDIA JENERALI HASHIM IDDI MBITA (MSTAAFU)
AMINA

 Imetolewa na Kurugenzi ya Habari na Mahusiano
Makao Makuu ya Jeshi, Upanga
S.L.P  9203,   Dar es Salaam,  Tanzania.
Kwa Mawasiliano zaidi: 0783 – 309963

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Saa 10 baada ya adhuhuri au alasiri

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...