Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI Bw. Jumanne Sagini
akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es
Salaam kuhusu baadhi ya Shule za Sekondari za Bweni zilizofungwa kutokana na ukosefu wa chakula ambapo
alisema shule hizo zimefungwa kimakosa kwani Serikali imeshapeleka fedha za
kununulia chakula kwenye halmashauri zote nchini. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu
Elimu TAMISEMI Bw. Zuberi Samataba.
Naibu Katibu Mkuu Elimu TAMISEMI Bw. Zuberi Samataba
akiwaeleza waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam mpango
wa Serikali kuajiri waalimu wa shule za msingi wenye elimu ngazi ya Stashahada
badala ya Cheti kama ilivyo sasa. Kulia ni Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu
TAMISEMI Bw. Jumanne Sagini.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI Bw. Jumanne Sagini
akiwaeleza waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam kuhusu
ajira kwa walimu wapya waliohitimu 2014/2015 na kutoa rai kwa waalimu hao
kwenda kuripoti kwenye vituo vya kazi watakavyopangiwa.
Baadhi ya
waandishi wa habari wakimsikiliza Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI Bw.
Jumanne Sagini wakati wa mkutano uliofanyika leo kwenye ofisi za TAMISEMI jijini Dar es Salaam. Picha na Fatma Salum (MAELEZO)
Hivi ni lini tutakuwa na aibu jamani? Shule zinafungwa kwa sababu hakuna chakula, wewe uliyekalisha makalio yako daresalam unaviambia vyombo vya habari kuseme zimefungwa kimakosa kwani chakula kipo. What the F...K (nimesahau kwamba luka hawezi kupost mpaka ubalozi wake umkubalie huko dc.
ReplyDelete