Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.
TANZANIA inatarajia kushiriki maonyesho ya nchi 149 ya bidhaa
za viungo ambapo watanzania 500 wanatakiwa kushiriki maonyesho hayo
yanayotarajia kuanza Mei 1 hadi 31 mwaka huu mjini Milan Italia.
Akizungumza na waandishi habari ofisini kwake katika viwanja
vya Mamlaka ya Maendeleo ya Tanzania(Tantrade),Jacqueline Maleko,amesema
maonyesho hayo ni fursa ya watanzania kujifunza mbinu mbalimbali za kutanua wigo wa biashara.
Jacqueline amesema kuwa Tantrade imefanya mawasiliano na katika
sehemu ya maradhi pamoja na mashirika ya ndege kwa kwa siku tano ambayo
itagharimu dola za Kimarekani 1500,hivyo watu mbalimbali wameombwa ili kuweza
kusogea mbele kiuchumi kutokana na elimu watakayoipta katika maonyesho hayo.
Amesema maonyesho haya yatalenga katika sekta ya chakula pamoja na
teknolojia mbalimbali duniani zitaendeshwa kwa kauli mbiu ya ,Kulisha Dunia
Nguvu ya Uhai.
“Hatuwezi kukua kiuchumi katika biashara za nje kwa kukaa
ndani bila kuweza kupata mawazo kutoka kwa nchi zilizo endelea kiuchumi katika
nyanja za maendeleo kutokana na biashara za nje”amesema Jacqueline.
Kwa upande wa Mkurugenzi wa Biashara za Nje,Anna Bulondo,amesema
maonyesho ya biashara ya mwaka huu yatakuwa ya aina yake kutokana na mbaoresho
mbalimbali na 24 hadi sasa zimedhibisha kushiriki maonyesho hayo.
Amesema katika mwaka huu watatoa tuzo kwa banda bora hivyo
wanatakiwa kufanya maresho ya mabanda hayo ili kuweza kupata tuzo hiyo. Viingilio katika maonyesho ya 39 ya biashara ya Kimataifa ya Dar
es Salaam vitakuwa sh.3000 kwa wakubwa na watoto Sh.1000.
Mkurugenzi Mkuu wa TANTRADE (katikati)
akizungumza katika mkutano wa maandalizi ya maonyesho ya 39 ya kimataifa
ulifanyika katika viwanja vya SabaSaba jijini Dar es Salaam leo.
Mkurugenzi wa Biashara za Nje,Anna Bulondo,
akizungumza katika mkutano wa maandalizi ya maonyesho ya 39 ya kimataifa
ulifanyika katika viwanja vya SabaSaba jijini Dar es Salaam leo.
Mkurugenzi wa Masoko na maendeleo akizungumza leo
katika viwanja vya Sabasaba na (kushoto)Mkurugenzi wa Biashara za
Nje,Anna Bulondo.
Baadhi ya wandishi wa habari waliohudhurika katika mkutano
wa maonyesho ya 39 ya biashara ya kimataifa,ulifanyika katika viwanja vya Saba
Saba jijini Dar es Salaam leo. (PICHA NA EMMANUEL MASSAKA,GLOBU YA JAMII).
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...