01
Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi Kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Richard Kayombo akitoa neno kuwakaribisha wageni katika mkutano wa Kwanza wa Wakuu wa Vyuo vya Kodi Afrika uliohudhuriwa na wajumbe zaidi ya 50 kutoka katika taasisi za kodi barani Afrika, Mkutano huo umeandaliwa kwa ushirikiano wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Taasisi za Kodi Afrika (ATAF), Jijini Dar es Salaam.
02
Mkuu wa Chuo cha Uongozi wa Kodi Tanzani (ITA) Prof. Isaiah Jairo akiongea na wajumbe wa mkutano huo na kueleza namna utakavyosaidia katika kuzijengea uwezo Taasisi za ukusanyaji kodi Afrika hivyo kuweza kuinua uchumi wa Mataifa mengi ya Afrika.
03
Mkurugenzi wa Ujengaji Uwezo kutoka Taasisi za Kodi Afrika (ATAF) Bw. Kennedy Onyonyi akiwaeleza wajumbe wa Mkutano huo namna Kamati hiyo inavyoshirikiana na Taasisi za Kodi Afrika katika kuzijengea Taasisi hizo uwezo wa Kiutendaji na kusaidia nchi wanachama kushiriki kuwa na sera ya pamoja ya masuala ya Kodi ili kuongeza ufanisi katika ukusanyaji kodi.
04
Naibu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Lusekelo Mwaseba Akiongea na wajumbe waliohudhuria Mkutano huo namna Tanzania ilivyofurahishwa na kuwa mwenyeji wa Mkutano huo wa Kwanza wa wakuu wa vyuo vya uongozi wa Kodi Afrika na kuwataka wajumbe kutumia fursa hiyo kujifunza masuala mbalimbali katika sekta hiyo ya ukusanyaji kodi kwani ni moja ya mhimili muhimu wa maendeleo kwa Mataifa mengi duniani.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...