Mwenyekiti
wa Chama wafanyakazi wa sekta ya usafirishaji
,Sharifu
Mohamed akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salam juu ya
wafanyakazi wa sekta hiyo kutojihusisha na migomo ,Kuhoto Katibu Mkuu
Salum Abdallaha TAROWU,kulia Mlezi wa TAROWU,Yakuub Rajabu (Picha na
Avila Kakingo wa Globu ya Jamii)
Na
Avila Kakingo,Globu ya Jamii.
CHAMA
cha wafanyakazi wa usafirishaji kwa njia
ya barabara Tanzania (TAROWU) kimewatahadharisha
wafanyakazi wa sekta ya usafirishaji kutojihusisha na mgomo katika sekta ya
usafirishaji.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa Chama
hicho,Sharifu Mohamed amesema wafanyakazi wa sekta ya usafirishaji wakijihusisha
katika migomo watasababisha kushuka kwa uchumi kutokana na sekta hiyo ilivyokuwa
muhimu.
Mohamed
amesema serikali inatakiwa kuchukua maamuzi magumu kwa wale ambao watahusika na
migomo ambayo inalenga kupoteza haki za wafanyakazi katika sekta hiyo.
Amesema
madai yanayotolewa na wafanyakazi wa sekta ya usafirishaji kuwa serikali
imeweka sheria ya kuwatoza madereva sh.550,000 hayana ukweli wowote ni viongozi
kutaka kuhalalisha mgomo huo.
Mohamed
amesema waajiri wanatakiwa kuwalipia gharama za mafunzo kwa madereva wao ili
waweze kufanya kazi hiyo kwa ufanisi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...