Mjasiriamali mahiri Afrika na Mkurugenzi Mtendaji wa Global Publishers Ltd, Eric Shigongo akitoa somo la ujasiriamali.
Wageni wakisikiliza somo la ujasiriamali kutoka kwa Shigongo.
Waimbaji wa GWT wakizidi kutoa burudani kwa washiriki wa Sunday Celebration Season 6.

KWA mara nyingine, kile Kikundi cha Kusifu na Kuabudu nchini cha Glorious Worship Team (GWT) Jumapili iliyopita kiliendelea na programu yake ijulikano kwa jina la 'Sunday Celebration' ambayo hufanyika kila Jumapili jioni.

Wiki iliyopita ilikuwa ni Sunday Celebration Season 6 ambapo burudani mbalimbali pamoja na elimu ya ujasiriamali vilitolewa kwa watu waliohudhuria katika Ukumbi uliopo Victoria Service Station, Mikocheni jijini Dar es Salaam.

Burudani ukumbini hapo ziliongozwa na Kundi la GWT likishirikiana na The Jordan Band huku elimu ya ujasiriamali ikitolewa na Mwalimu mahiri wa Ujasiriamali Afrika ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Global Publishers Ltd, Eric Shigongo.(PICHA ZOTE NA GWT).
PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...