Katika mwendelezo wa kipindi cha ‘Ubishi - Komaa Upate Pesa’, wiki hii Bwana Costantine Magavilla anakuletea sehemu ya pili iitwayo ‘Kazi ni Tabia’. Kazi ni gumzo kwa vijana wengi wa mjini ila ni kitu gani kinacho wachochea vijana kufanya kazi haswa na je madhara yake ni nini kwao.
Pata majibu kwa kutembelea www.magavilla.comau kwa kubofya hapa https://www.youtube.com/watch? v=PY-QUloAZXY
Usikose kufuatilia vipindi hivi vinavyolenga kuelimisha, kukuhamasisha utazame upya maisha yako upateujasiri wa kubadili fikra na kufanya yako kila wiki siku ya Jumanne.
Bwana Costantine Magavilla ni mwandishi wa kitabu kiitwacho 'Life and You' na ni mhamasishaji maarufu Tanzania katika makongamano mbalimbali kuhusiana na maendeleo binafsi na mabadiliko ya kibiashara. Ni mdau mkubwa wa masuala ya masoko hususan katika kutangaza biashara na miongoni mwa kazi zake ni kuwahamasisha vijana kujituma na kuchangamkia fursa.
Nadhani neno tabia hapo unamaanisha wito (msukumo ni hiyo kazi si matokeo ya kazi). Na hapo ndo kujituma, ufanisi, n.k. hutokea. Lakini wale wasio na wito ndo unakuta rushwa, ufisadi, ubaguzi, uonevu, n.k.
ReplyDeleteElimu pia ni wito. Wasio na wito wakihitimu huwa mbmbumbu baada ya miaka 5.
Lakini wenye wito huendelea kujielimisha mpaka pumzi ya mwisho.