Na Avila Kakingo,Globu ya jamii

MAMLAKA ya Mapato Nchini (TRA), kwa kipindi cha miezi miwili iliyopita imekusanya zaidi ya Sh. Bilioni 258 zilizotokana na faini ya bidhaa mbalimbali za magendo.

Hayo ameyasema leo Mkurugenzi huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi wa TRA, Richard Kayombo wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo jijini Dar es salaam,amesema TRA inaungana na jeshi la Polisi katika kukamata watu wanaojihusisha na usafirishaji na uuzaji wa bidhaa za magendo ambazo zinaisababishia serikali kukosa mapato.

Amesema kwa Mkoa wa Kagera zaidi ya Sh.milioni 120 zilizotokana na pombe ya aina ya signature Vodka katoni 2043 kutoka nchini Uganda sawa na lita 24,516 yenye thamani ya zaidi ya sh.milioni 61, zilizosafrishwa kwa jahazi la MV Tabasamu lenye namba za usajili MTZ 0541.

Hata hivyo amesema Mkoa wa Morogoro kodi ya zaidi ya Sh.milioni 66 ilipatikana baada ya kukamata madumu 1599 ya lita 20 za mafuta ya kupikia yenye thamani ya zaidi ya sh.milioni 65 ambapo wakwepa kodi hao walilipa faini pamoja na kodi waliyokuwa wakikwepa na Mkoa wa Tanga madumu 888 ya mafuta ya lita 20 yalikuwa na thamani ya zaidi ya sh.milioni 15 yaliyokamatwa eneo la Kwame katika bandari bubu ya wilayani Mkinga.

Kayombo amesema katika Mkoa wa Arusha jumla ya lita 2290 za mafuta ya taa zenye thamani ya zaidi ya sh.milioni mbili,mafuta hayo yalikuwa yakisafirishwa kwa gari aina ya Toyota hiace iliyokuwa ikisafirishwa kutoka Holili Kwenda Mkoani Moshi.
Mkurugenzi huduma na elimu kwa mlipa kodi,Richard Kayombo akizungumza leo na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akiwataka wananchi kutoa taarifa ya bidhaa zinazosafirishwa kwa njia za magendo, katika ukumbi wa Idara ya habari MAELEZO,jijini Dar es Salaam. kushoto ni Meneja elimu kwa mlipa kodi,Diana Masala na kulia ni Mkurugenzi msaidizi Idaya ya habari Maelezo Zamaradi Kawawa.(Picha na Avila Kakingo).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...