Pamoja na Tume ya  Taifa ya Uchaguzi kuahirisha  tarehe ya kupiga kura ya maoni, Shirika la Kimataifa linaloshughulikia Elimu na Utamaduni (UNESCO), kwa kushirikiana na Kampuni ya Focus Media pamoja na Mtandao wa radio za jamii  (COMNETA), limeamua kusambaza Katiba inayopendekezwa kwa njia ya sauti nchi nzima, ili wananchi wapate elimu  kuhusu maudhui yaliyomo ndani ya Katiba na kufanya maamuzi sahihi pindi siku ya kupiga kura itakapowadia. 

Aidha, mkakati huo wa kusambaza Katiba inayopendekezwa kwa njia ya sauti unajumuisha utoaji elimu kuhusu mfumo mpya wa kujiandikisha kwa njia ya kieletroniki (Biometric Voters Registration – BVR) pamoja na kuhamasisha wananchi ili wajitokeze kwa wingi kujiandikisha na kutimiza haki yao ya kikatiba wakati wa upigaji kura.

Akipokea, nakala za CD zenye Katiba inayopendekezwa kwa njia ya sauti, Mkurugenzi Mkaazi wa UNESCO nchini Tanzania Bi Zulmira Rodrigez, alipongeza Kampuni ya Focus Media kwa kuandaa matoleo hayo na kusisitiza radio za jamii kuzitumia ili kuwaelimisha wananchi mikoa yote juu ya Katiba inayopendekezwa.

 “Nimefurahi sana kuona hizi nyenzo za kisasa kama SD cards, kwa sababu tunaonesha kwamba radio za jamii ni njia bora zaidi za kutoa taarifa na pia zinawezesha kupata mrejesho kutoka kwa wananchi.”

Bi Zulmira Rodrigez, ameongeza kusema “Hili ni jambo zuri sana kwa jamii, na inapeleka taarifa mpaka katika njia ya chini kabisa, vijiji vilivyoko ndani kabisa.”  

Mwenyekiti wa mtandao wa redio za jamii Bwana Joseph Sekiku amewashuri watangazaji wa redio mbalimbali wliohudhuria semina hiyo amewaasa kutumia muda uliobai wa siku28 vizuri ili kuelimisha jamii maudhui ya Katiba inayopendekezwa ili wananchi wafanye maamuzi sahihi katika kura ya maoni na uchaguzi mkuu.

Sekiku ameongeza kwamba kwa sasa itapatikana kupia Focus Media pro ltd kwa kupitia mitandao yote ya kijamii na redio mtandao na wananchi wanaweza kuwasiliana kwa kutuma ujumbe mfupi kupitia namba +255 772 55 55 53
Mkurugenzi Mkaazi wa UNESCO nchini Tanzania Bi Zulmira Rodrigez akisikiliza jambo kutoka kwa Mwenyekiti wa mtandao wa redio za jamii Bwana Joseph Sekiku.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. mimi hapa ndio huyashangaa haya mashirika ya umoja wa mataifa wao ndio wa kwanza kupiga kelele kutetea haki, uwazi na unyanyasaji pia wana wawakilishi wao karibu nchi zote ikiwemo hapa Tanzania sasa kuna umuhimu gani wameona au kugundua kuwa hii katiba pendekwa kuwa ni ya wananchi sio ya ccm ina maana hawakuona yale yote yaliyofanywa kupitisha katiba ya ccm hii haikuhitaji utaalamu kujua ccm walikuwa na jukumu la kuigharimia wenyewe hii kazi sio kutafuta wafadhili kwa kuipigia debe katiba ya chama cha siasa.maoni yangu tusiyategemee mashirika haya kusimamia haki wao wako nchini kwa kushirikiana na utawala au chama tawala hata kama wanajua sheria zinavunjwa hiyo sio kazi yao ndio maana hufanya kazi pia na madikteta ulimwenguni tatizo wasiji pigie debe kuwa mashirika yao ni ya kusimamia usawa haki za watu na sheria ikiwa wao ni wadau wakubwa wa kuzipuuza.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...