Zaidi
ya asilimia 60 ya watoto wenye umri wa miaka 13 hadi 17 wanatumia zaidi ya
masaa mawili kila siku kuangalia mitandao ya kijamii pamoja na vipindi
mbalimbali vya Televisheni. Hii inaweza kuwa njia kubwa ya kuunganisha, lakini
pia kuna hatari zinazohusiana na kutumia muda mwingi sana kwenye vyombo vya
habari kijamii.
Leo hii ni nadra kukuta familia
ambazo watoto na vijana wake hawajaathirika na vyombo vya habari na elektroniki
kama vile televisheni, intaneti na michezo mingine tofauti ya kompyuta.
Hata hivyo utumiaji mkubwa na wa
masaa mengi wa vyombo hivyo hauwahusu watoto na vijana tu, bali watu wazima pia
wameathirika na jambo hilo.
Kutokana na sababu kadhaa za kimwili,
kisaikolojia na kiroho, kuna udharura kwa watoto kusimamiwa vyema na wazazi,
mashirika na taasisi za kielimu na kiutamaduni na kadhalika vyombo vya habari
ili kupunguza madhara yanayotokana na matumizi mabaya ya vyombo hivyo vya
elektroniki. Licha ya kompyuta kuwa na pande
chanya tofauti za kimaendeleo, hasa katika nyanja za kielimu na huduma za
mawasiliano, lakini chombo hicho pia kina nafasi hasi kwa watoto na hata kwa
watu wazima.
Utumiwaji usio na udhibiti wa chombo
hicho na kadhalika vyombo vingine vya elektroniki kama vile televisheni,
unaweza kuyaweka hatarini maisha ya watoto kutokana na athari zake mbaya kwa
ustawi wa kiroho, kisaikolojia na kijamii wa watoto hao.
Harakati zetu za kifizikia na
miamala yetu tofauti ya kijamii, ni umuhimu yenye taathira kubwa kwa afya na
tabia za mtoto. Kinyume chake, ikiwa mtoto atatumia muda wake mwingi katika
matumizi ya michezo ya kompyuta, basi hawezi kunufaika na upande chanya wa
kujenga akili yake wala harakati bora kwa ajili ya kuufikia ukamilifu wake
kijamii.
Mbali na hayo, watoto pia wanaweza
kukabiliwa na hatari ya kutekeleza vitendo vya ukatili na visivyo vya kikatili
hata katika umri wao mdogo. Hali hiyo ambayo inaweza kufikiwa ghafla au hata
kwa makusudi, huwaletea watoto na vijana madhara yasiyoweza kufidika hasa
kuhusiana na masuala ya kiafya, kisaikolojia sambamba na kueneza kwa kiasi
kikubwa matatizo ya kimwili na kiakili kama vile utovu wa maadili, vitendo vya
ukatili, madawa ya kulevya, tabia mbaya katika jamii, kuzorota thamani za
familia na kuenea jinai na uhalifu wa kila aina katika jamii.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...