Mkuu wa Wilaya Ilala, Raymond Mushi (katikati) akizungumza katika siku ya kilele cha maadhimisho ya uboreshaji mazingira ya shule za msingi na sekondari za halmashauri ya manispaa ya Ilala, yaliyofanyika katika viwanja vya Mnazimmoja Jijini Dar es Salaam leo. (kushoto) Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, Isaya Mugurumu(kulia) ni Mwenyekiti kamati ya uchumi na huduma za Jamii Manispaa ya Ilala Angelina Malembeka.
0Kikundi Mganda cha shule ya Msingi Umoja ya Manispaa ya Ilala kikitoa burudani katika maadhimisho ya uboreshaji mazingira ya shule za msingi na sekondali za halmashauri ya manispaa ya Ilala.
Baadhi ya Waalimu na Wanafunzi wa shule za Msingi na Sekondari wakiwa na kombe lao la ushindi wa utunzaji wa mazingira, katika maadhimisho ya uboreshaji mazingira ya shule za msingi na sekondali za halmashauri ya manispaa ya Ilala.PICHA NA EMMANUEL MASSAKA.
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.
MKUU wa Wilaya Ilala Raymond Mushi ametaka usafi wa Mazingira uendane na utoaji wa elimu bora kwa kuweka mazingira rafiki ya kufundishia wanafunzi
Mushi aliyasema hayo leo wakati wa maadhimisho ya uboreshaji wa Mazingira katika Shule Msingi na Sekondari kwa Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam,Mushi amesema mazingira rafiki kwa wanafunzi yanawafanya kupenda shule na kuachana na utoro pamoja kuongeza ufaulu katika mitihani ya taifa.
Mushi amesema asasi pamoja na idara za sekta ya umma kuhakikisha suala la elimu ya mazingira na usafi linapewa kipaumbele katika maeneo yao ya kazi . Aidha amesema kila mtu kwa nafasi yake anatakiwa kushiriki kikamilifu katika uhifadhi wa mazingira kulingana na sheria zinavyoelekeza na watu waliopewa mamlaka ya kusimamia mazingira kuhakikisha zinafanya kazi kwa bidii.
Mushi amesema madhara yakitokea kutokana na uchafu wa mazingira waadhirika ni wote hivyo ni vyema kila mtu afanye usafi kwa nafasi yake bila kumsubiri mtu mwingine.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...