Kanali Mstaafu Joseph Leon Simbakalia.
===== ====
UTEUZI WA MWENYEKITI WA BARAZA LA TUME YA TAIFA YA SAYANSI NA TEKNOLOJIA (COSTECH)
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikiwete, amemteua Mhandisi, Kanali Mstaafu Joseph Leon Simbakalia, kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Tume ya
Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) kwa kipindi cha miaka mitatu kuanzia tarehe 10 Aprili 2015.
Uteuzi huo ni kwa mujibu wa Kifungu Na. 4 cha Sheria Na. 7 ya Mwaka 1986 iliyounda Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia. Mhandisi Kanali Mstaafu Joseph Leon Simbakalia kwa sasa ni Mkurugenzi Mkuu wa Export Processing Zones Authority (EPZA).
Imetolewa na:
John Mngodo
KAIMU KATIBU MKUU
Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...