Mkuu wa Oganaizesheni wa
NCCR-Mageuzi,Faustine Sungura akizungumza na Wandishi wa habari katika Makao
Makuu ya Chama cha NCCR-Mageuzi,leo jijini Dar es Salaam,(kushoto) ni Katibu wa Vijana wa Chama cha NCCR-Mageuzi Taifa Mawazo Atanas.
Mkuu wa Oganaizesheni wa NCCR-Mageuzi, Faustine Sungura akimkabidhi fomu ya kugombea nafasi ya Urais Katibu wa vijana wa chama cha NCCR-Mageuzi taifa Mawazo Atanas kwa niaba ya Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam,Dk George Mihango,jijini Dar es Salaam leo.
Baadhi ya waandishi wa
habari waliohudhuria katika mkutano wa kumkabidhi fomu ya kugombea nafasi ya
urais Katibu wa Vijana wa Chama cha
NCCR-Mageuzi Taifa,Mawazo Atanas kwa niaba ya Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es
Salaam,Dk.George Mihango,leo jijini Dar es Salaam. (Picha na Avila Kakingo,Globu ya
Jamii)
Na Avila Kakingo,Globu
ya Jamii
UMOJA wa Vijana wa Chama cha
NCCR-Mageuzi wamemchukulia fomu ya
kugombea nafasi ya Urais kwa chama hicho,Dk.George Mihango ambaye ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari katika
Makao Makuu ya Chama hicho, leo jijini Dar es Salaam,Mkuu wa Oganaizesheni wa
NCCR-Mageuzi, Faustine Sungura,amesema vijana wa chama hicho wamemshawishi
Mhadhiri huyo kwakuwa anavigezo vyote vya kugombea nafasi hiyo.
Sungura,amesema kuwa milango
iko wazi kwa wanachama kuja kuchukua fomu za kugombea nafasi mbalimbali katika
chama hicho katika uchaguzi unaotarajia kufanyika hivi karibuni.
Aidha amesema,wakati umefika kwa vijana waliozaliwa baada ya uhuru sasa
wanaweza kugombea nafasi za uongozi katika chama hicho, kutokana na uwezo wanaonyesha katika vitu mbalimbali.
Nae Katibu wa Vijana wa Chama cha NCCR- Mageuzi Taifa,Mawazo Atanas
amewashukuru vijana wa chama hicho kwa kusaidia kumchagua Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam,Dk.George Mihango
kuchukua fomu kwaajili ya kugombea nafasi ya Urais katika chama hicho ambaye atachuana na wagombea mbalimbali katika nafasi hiyo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...