Mwakilishi wa Vijana kutoka kamati ya kudhibiti Ukimwi manispaa ya Shinyanga Bw,Rigobert Rwehumbiza akielezea wajibu binafsi kwa kijana kwa washiriki wenzie katika warsha ya siku nne ya stadi za maisha na afya ya uzazi.
Katibu
asasi ya Vijana ya Boys & Girls Bw,Johnson Jacob kutoka Bariadi
akionyesha igizo lilikuwa likionyesha wajibu wa Vijana kwa Familia
ikiwamo kuwalinda na kuwapatia mahitaji yao muhimu.
Mtaalamu
wa Stadi za Maisha Bw,Robert Semkiwa akiwafundisha waratibu wa ukimwi
na maafisa Vijana wanaohudhuria Warsha ya siku tatu inayohusu Stadi za
maisha na Afya ya uzazi jinsi ya kukabiliana na Msongo wa Mawazo na njia
gani za kutumia kukabiliana nao.
Waratibu
wa Ukimwi na maafisa Vijana wakiwa katika mjadala wa pamoja
wakipambanua kwa kina stadi mojawapo katika stadi tatu za maisha ya
kujitambua leo jijini Mwanza.kundi ili lilikuwa likijadili jinsi ya
kukabili mihemko kwani ni hatua mojawapo kijana anayoipitia katika
maisha yake.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...