Mtafiti wa Lugha za alama Profesa Henry Muzare akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo katika ukumbi wa habari MAELEZO,kuhusiana na umuhimu wa lugha za alama kwa viziwi na jamii,(kulia) Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Viziwi Tanzania (CHAVITA)Dicksom Mveyange.
Mkalimani wa Lugha za alama Octaviani Simba akimtafsiria lugha za alama  Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Viziwi Tanzania (CHAVITA),Dicksom Mveyange,leo katika ukumbi wa habari MAELEZO jijini Dar es Salaam.
(Picha na Avila Kakingo,Globu ya Jamii)
Na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.
CHAMA cha viziwi Tanzania(CHAVITA),waomba ushirikiano kwa jamii kuwasaidia watu wenye uziwi kwa kuwa wengi huwatenga kutokana na kutoelewa vitu vinavyoendelea.
Hayo yamesemwa na  Mtafiti wa Lugha za alama profesa Henry Muzare wakati akizungumza na wandishi wa habari kuhusiana na umuhimu wa Lugha za alama kwa viziwi na jamii zima leo katika ukumbi wa habari MAELEZO  jijini Dar es Salaam.
Muzare alisema luwa binadamu anahaki ya kutumia lugha anayoimudu ili kuwasiliana na watu wenginekatika jamii, lugha hizo ni pamoja na alama  wanazozitumia viziwi.
Vitendo vyovyote  vinavyomnyima mtu fursa ya kutumia lugha anayoimudu vizuri inatafsiriwa ni kumnyanyasa alisema  Muzare.
Muzare amesema kuwa  katika mfumo wa elimu ya mjumuisho unaotumika  kwa kuwachanganya viziwi na wanaosikia bila kuwa na msaada au huduma yeyote hali hiyo inawafanya watu wenye uziwi  kuishi maisha ya kubahatisha, pia hali hiyo inakatisha tamaa kwa watu hao wakiwa shuleni na chuoni, kwa kuwa walio wengi hawaelewi mambo yanayofundishwa.
Aliongezea kuwa kwenye huduma za kijamii kama hospitali, mahotelini, sokoni hata kwenye vyombo vya mawasiliano mfano luninga,watu wenye uziwi wanahitaji mkalimani ili kupunguza hali ya watu hao kukosa haki zao za lugha yao wanayoielewa kwa ufasaha.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...