Na Bashir Yakub.
Upangaji kama upangaji una mambo mengi. Hii ndio sababu sheria imegusa eneo hilo pia. Kila mtu anajua kuwa upangaji si lazima uwe wa nyumba ya kuishi tu bali hata ule wa maeneo ya biashara pia. Ipo misuguano mingi ambayo hutokea katika miamala ya upangaji na upangishaji. Ipo misuguano inayotokana na ukorofi tu lakini ipo misuguano inayotokana na kutojua baadhi ya mambo ya msingi na ya kisheria kuhusu dhana nzima ya upangaji na upangishaji . Leo nitaeleza mambo mawili tu kuhusu upangaji na upangishaji.
1.INARUHUSIWA KUPANGA NA WEWE UKAMPANGISHA MWINGINE.
Sheria haimkatazi mtu kupanga sehemu halafu naye akaamua kumpangisha mwingine. Hili lipo na si kinyume cha sheria kufanya hivi. Na zaidi hata huyu aliyepangishwa naye anaweza kumpangisha mwingine wa tatu. Yaani ikawa A amempangisha B na B amempangisha C na C amempangisha D na wote katika eneo hilohilo.
Hii yote inaruhusiwa na upangaji wa kila mmoja unalindwa na sheria na kila mmoja anapata haki zake kwa nafasi yake. Kwa mfano kila mpangishaji ataitwa mwenye nyumba yaani A ataitwa mwenye nyumba na B na B ataitwa mwenye nyumba na C na C ataitwa mwenye nyumba na D. Halikadhalika kila aliyepangishwa ataitwa mpangaji.
Suala la msingi sana katika upangaji wa namna hii ni kuwa ule mkataba wa mwenye nyumba halisi ambaye ni mmiliki kabisa yule A uwe unatoa ruhusa kwa mpangaji aliyempangisha naye kuruhusiwa kupangisha mwingine na yule mwingine naye mkataba wake umruhusu kumpangisha mwingine na mwingine naye mkataba wake umruhusu kumpangisha mwingine iwe hivyohivyo. Ikiwa mkataba wa mmoja haumruhusu kupangisha zaidi basi huyo asiyeruhusiwa hawezi kumpangisha mwingine na akifanya hivyo itakuwa kinyume cha sheria. Kisichowezekana ni kuwa huwezi kuwa mpangaji halafu ukampangisha mwingine bila kuwa umeruhusiwa kufanya hivyo na mwenye nyumba katika mkataba wenu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...