Mchezo no.91 wa Kombe la Shirkisho barani Afrika (CC) hatua ya 16 bora uliofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es salaam, kati ya wenyeji timu ya Young Africans dhidi ya Etoile du Sahel kutoka Tunisia umeingiza jumla ya sh. 223,135,000.

Jumla ya watazamaji 36,105 walikata tiketi kuhudhuria mchezo huo, huku VIP A zikikatwa tiketi 68, VIP B tiketi  869, VIP C tiketi 582, Orange tiketi 1,955 na viti vya rangi ya Bluu na Kijani tiketi 32,631 ziliuzwa.

Mgawanyo wa mapato ni VAT 18% sh. 34,037,542.37, Gharama ya tiketi sh. 11,462,000, Gharama ya Uwanja 15% sh. 26,645,318.64, Gharama za mchezo 15% sh. 26.645,318.64, CAF 5% sh. 8,881,772.88, TFF 5% sh. 8,881,772.88 na Young Africans 60% sh. 106,581,274.58.

IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...