Na Mwandishi Wetu
Kampuni ya Kimataifa ya Zest imezindua simu mpya zenye huduma zote muhimu kwa bei nafuu.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa simu hizo jijini Dar es Salaam, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni hiyo, Salum Awadh amesema kuwa simu hizo ambazo ni imara zitauzwa kwa bei nafuu ili kila mtu aweze kununua.
"tumeingiza sokoni simu mpya aina ya 7 Mobile ambazo zina huduma za mitandao ya kijamii ikiwemo Internet, Whatsap pamoja na Facebook huku bei yake ikiwa ni 35,000, aina nyingine ni Tablet inayojulikana kwa jina la ZestPad Tango ambayo inauzwa sh. 165,000.
Aidha aliongeza kuwa mbali ya huduma muhimu za kijamii kama facebook pamoja na whatsap simu hizi pia wakati unachaji zinapojaa zinajizima zenyewe.
"Tunameamua kuingiza sokoni simu zenye ubora wa hali ya juu ili kila mtu aweze kutumia simu za kisasa zenye gharama nafuu" alisema Mkurugenzi huyo".
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Zest International, Salum Awadh akionyesha Tablet wakati wa uzinduzi wa aina mpya za simu uliofanyika jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki. Kushoto ni Meneja wa Kampuni ya Jumia, Michael Ryoba na Meneja Maendeleo ya Biashara, Rajab Smith. (Picha na Francis Dande).
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Zest International, Salum Awadh akionyesha Tablet ambayo inauzwa kwa shilingi 165,000.
Meneja wa Kampuni ya Jumia, Michael Ryoba akifafanua jambo kwa waandishi wa habari.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...