JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
BUNGE LA TANZANIA
1.0
UTANGULIZI
Mkutano wa
Ishirini (20) wa Bunge la Kumi (10) unatarajia kuanza mjini Dodoma tarehe 12
Mei 2015. Mkutano huo ambao ni mahususi kwa ajili ya kujadili na kupitisha
Bajeti ya Serikali ndiyo utakaokuwa mkutano wa mwisho wa Bunge hili kabla ya kuvunjwa
na baadaye kufanyika Uchaguzi Mkuu mwezi Oktoba 2015.
Hivyo, Wabunge
wote wanapaswa kuwa wamewasili mjini Dodoma ifikapo Jumapili tarehe 10 Mei 2015 tayari kuhudhuria
kikao cha briefing siku ya Jumatatu
tarehe 11 Mei, 2015.
2.0
SHUGHULI
ZITAKAZOTEKELEZWA
Katika
Mkutano huu kutakuwa na wastani wa maswali 295 ya msingi yatakayoulizwa na
kupatiwa majibu. Aidha, kutakuwa na wastani wa maswali 56 atayoulizwa Waziri
Mkuu na kuyapatia majibu kwa mujibu wa Kanuni ya 38(1) ya Kanuni za Kudumu za Bunge Toleo la Aprili 2013.
Aidha, katika
mkutano huo, taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ya
mwaka 2013/2014 itawekwa mezani na kufuatiwa na taarifa yenye majibu kuhusu
hoja zilizotolewa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa
Hesabu za mwaka wa Fedha wa 2013/2014.
Baada ya
hayo, Bunge litapokea na kujadili utekelezaji wa Wizara zote 24 wa Bajeti kwa
mwaka wa Fedha unaoisha pamoja na Makadirio na Matumizi ya Serikali kwa mwaka
wa Fedha 2015/2016.
Siku ya
Alhamisi tarehe 11/Juni/2015 saa 4:00 (nne) asubuhi Waziri anayehusika na Mipango atawasilisha
taarifa ya Hali ya Uchumi wa Nchi, ikifuatiwa na hotuba ya Bajeti ya Serikali
kwa mwaka wa fedha 2015/2016 itakayosomwa na Waziri wa Fedha saa 10:00 jioni. Wabunge wote mnaombwa kuwepo Dodoma.
Mjadala wa hotuba
ya Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa Fedha wa 2015/2016 utaanza na utafuatiwa na
kupitishwa kwa Muswada wa Sheria ya Matumizi wa Mwaka 2015 pamoja na kujadili
na kupitisha Muswada wa Sheria wa Fedha wa Mwaka 2015.
3.0 SHUGHULI
NYINGINE
Shughuli za Mkutano
wa 20 zinatarajiwa kumalizika tarehe 27 Juni, 2015 na kuhitimishwa kwa hotuba
ya Waziri Mkuu ya kuliahirisha Bunge.
Ratiba kamili
ya shughuli za Mkutano wa Ishirini wa Bunge la Kumi itapatikana kwenye Tovuti
ya Bunge ambayo ni www.parliament.go.tz
Imetolewa na:
Ofisi ya Bunge,
Idara ya Habari, Elimu kwa Umma na
Uhusiano wa Kimataifa,
DAR ES SALAAM
08 Mei 2015
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...