Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini Mh. Radhia Msuya (katikati)  katika picha ya pamoja na waoneshaji kutoka taasisi za serikali katika maonesho ya INDABA AFrika Kusini. Wa pili kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mwendeshaji wa Bodi ya Utalii Tanzania bii Devota Mdachi.
Waoneshaji kutoka tasisi za Serikali katika maonesho ya INDABA Durban Afrika Kusini wakiwa kazini kuitangaza Tanzania.

Na: Geofrey Tengeneza.
Banda la Tanzania katika maonesho ya Kimataifa ya INDABA yaliofanyika katika jiji la Durban nchini Afrika Kusini lilikuwa miomgoni mwa mabnda yaliyon’gara zaidi kwa kuvutia watu waliotembelea maonesho hayo ambayo kwa mwaka huu yalifanyika kwa siku tatu kuanzia 9 hadi tarehe 11/5/2015.

Katika maonesho hayo ambayo ni makubwa zaidi barani Afrika na ya tatu kwa ukubwa duniani baada ya ya yale ya ITB Ujerumani na WTM Uingereza Tanzania iliwakilishwa na makampuni 30 zikiwemo pia taasisi za Serikali kama vile TTB, Tanapa na Ngorongoro.

Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini Bibi Radhia Msuya alipata fursa ya kutembelea maonesho hayo na kuzungumza na waoneshaji kutoka Tanzania na kuwapongeza kwa namna walivyojipanga kushirki katika maonesho hayo chini ya uratibu wa Bodi ya Utalii Tanzania –TTB.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 12, 2015

    Nguo ya Balozi inatangaza utalii.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...