Na Pamela Mollel, Arusha
Kufuatia anguko la shilingi ya Tanzania dhidi ya dola wafanyabiashara nchini wametakiwa kuona kuwa ni fursa ya wao kijiinua kiuchumi katika biashara zao ndani na nje ya nchi na kuachana na propaganda za wanasiasa ambapo wanalalamikia anguko hilo.
Ambapo hali hiyo imesababisha kupanda kwa bidhaa mbalimbali nchini hali inayotajwa kuongeza ugumu wa maisha ya wananchi sambamba na wafanyabiashara nchini ambao wananunua na kuagiza bizaa kutika nje ya nchi. Hayo yameelezwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dk. Charles Kimei wakati akiongea na waandishi wa habari wakati akitoa taarifa ya mkutano mkuu wa ishirini wa wanahisa wa Benki ya Crdb unatarajia kufanyika kesho jijini Arusha katika kituo cha mikutano cha Kimataifa AICC.
Hata hivyo alisema kuwa hivi sasa Benki hiyo imeweza kupata faida ya shilingi bilioni 95.6 sawa na asilimia 14 kwa mwaka 2014 ambapo limekuwa ni ongezeko kubwa zaidi kutokea ambapo faida hiyo itawasaidia kuweza kupatia wanahisa hao gawio la shilingi 15 kwa kila hisa na idadi ya wanachama hao. Ambapo mizania imeongezeka kwa asilimia 17 katika lengo lao katika mwaka huu ingawa soko limekuwa gumu kutokana na mfumuko wa bei uliopo sasa.
Dk. Kimei aliongeza kuwa kutakuwepo na ajenda mbalimbali katika mkutano huo mkuu ambapo moja ya ajenda ni kuangalia namna ya kukua zaidi na kuongeza mtaji wao na kuboresha mfumo mzima wa Tehama ili kuweza kukabiliana na wizi wa kupitia mtandao ili kuweza kuwahakikishia usalama wa pesa za wateja wao.
Aidha Banki hiyo inamkakati wa kuongeza mtaji wao ambapo wanatarajia kuongeza zaidi ya billion 100 ili kuongeza aman za banki na mtaji wao ili kuboresha huduma hizo na kukuza rasilimali za banki hiyo.
Dk. Kimei aliongeza kuwa wanamkakati wa kupanua huduma zao katika nchi ya Burundi na nchi jirani ili kuweza kuwarahishishia wateja wao pindi wanapotoka na kutembelea nchi hiyo na kupata huduma ya miamala ya fedha.
Benki hiyo hivi sasa wanamawakala zaidi ya 575 ya fahari huduma na wanamashine ya zaidi ya 375 za kutolea pesa katika mikoa yote nchini ili kuwarahisishia wateja wao kupata huduma za kibenki.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akiongea na waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari jijini Arusha akitoa taarifa ya mkutano mkuu wa ishirini  wa wanahisa wa Benki ya CRDB  unaotarajia kufanyika May 8  jijini Arusha.
SAM_2456Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei, akizungumza na waandishi wa habari. Kushoto ni Naibu Mkurugenzi Mtendaji Huduma Mtambuka Benki ya CRDB Bi.Esther Kitoka na kulia ni Naibu Mkurugenzi Mtendaji Uendeshaji na Huduma kwa Wateja Benki ya CRDB, Saugata Bandyopadhyay
SAM_2443Baadhi ya waandishi wa habari kutoka jijini Arusha wakiwa katika mkutano huo.
SAM_2437Meneja Mahusiano wa Benki ya CRDB, Godwin Semunyo akiwa katika mkutano huo.
SAM_2432Mkurugenzi wa Masoko,Utafiti na Huduma kwa Wateja, Tully Esther Mwambapa akiongea katika mkutano na waandishi wa habari katika maandalizi ya mkutano mkuu wa ishirini wa wanahisa wa Benki ya CRDB.
Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...