BENKI ya EximTanzania imezindua kampeni inayolenga kuwahamasisha wateja wake juu ya matumizi ya kadi zake mpya za ‘Faida Chip and PIN Debit card’ ambazo zimeundwa kwa kuzingatia vigezo vya kiusalama zaidi.
Kwa mujibu wa Meneja Bidhaa wa benki hiyo Bw. Aloyce Maro hatua hiyo ni sehemu ya jitiahada za benki hiyo kuhakikisha kwamba huduma zake zinatolewa kwa uhakika na usalama zaidi kwa faida ya wateja wake.
“Lengo kubwa la kampeni hii ni kuwahamasisha wateja wetu juu ya matumizi ya kadi zetu mpya za ‘Faida Chip and PIN Debit card’ ambazo zinatumia ‘chip’ badala ya ‘magnetic strip’ lengo likiwa kuongeza usalama wa akaunti za wateja wetu’’ alisema Bw. Maro wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo jana jijini Dar es Salaam.
Matumizi ya kadi hizo yanaelezwa kuongeza usalama na amani miongoni mwa watuamiaji wake kwa kuwa zina uwezo wakipekee katika kuhifadhi na kutambua taarifa za mtumiaji na hivyo kuondoa hofu ya wizi wa namna yoyote ile, kwa mujibu wa Bw. Maro.
“Kadi hii inauwezo mkubwa wa kuhifadhi taarifa pamoja kumtambua mmiliki wake.Uwezo huu ndio siri ya mafanikio yake kwa kuwa inauwezo wa kuwazuia kabisa watu wenye nia ovu na akaunti ya mteja hususani kwa kufanya jaribio la namna yoyote la wizi,’’ alisema Bw. Maro.
Akiizungumzia zaidi kadi hiyo Bw. Maro alisema inauwezo wa kumuwezesha mtumiaji wake kuweza kuifikia akaunti yake na kufanya miamala kutoka kwenye mashine za kutolea fedha zenye uthibitisho wa ‘MasterCard’ pamoja na zile za POS ulimwenguni kote bila usumbufu wowote.
Aidha Bw. Maro aliwahamasisha wateja wa benki hiyo ambao bado hawajachukua kadi zao wajitokeze kuzichukua kwenye matawi ya benki hiyo ili waanze kufaidi matumizi yake.
Meneja
Bidhaa wa Benki Ya Exim Tanzania, Aloyse Maro (kulia) akisisitiza jambo
wakati wa mkutano wa waandishi wa habari kutangaza uzinduzi wa kampeni
mpya ya benki hiyo inayolenga kuhamasisha wateja juu ya matumizi ya kadi
mpya ya Faida Debit Card, ambayo imeimarishwa zaidi kiusalama, jijini
Dar es Salaam jana. Wanaoshuhudia ni Meneja Masoko Msaidizi wa benki
hiyo, Anita Goshashy (kushoto) na Zawadi Kanyawana kutoka kitengo cha
Huduma za Rejareja za Kibenki (katikati)
Meneja
Bidhaa wa Benki Ya Exim Tanzania, Aloyse Maro (katikati)akizungumza na
waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa mkutano wa waandishi wa
habari kutangaza uzinduzi wa kampeni mpya ya benki hiyo inayolenga
kuhamasisha wateja juu ya matumizi ya kadi mpya ya Faida Debit Card,
ambayo imeimarishwa zaidi kiusalama, jijini Dar es Salaam jana.
Wanaoshuhudia ni Meneja Masoko Msaidizi wa benki hiyo, Anita Goshashy
(kushoto) na Zawadi Kanyawana kutoka kitengo cha Huduma za Rejareja za
Kibenki (kulia).
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...