BG Tanzania imetangaza kutoa udhamini kwa wanafunzi 13 wa shahada ya uzamili ya sayansi ya mafuta na gesi (MSc. in Petroleum Geology) itakayotolewa katika Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Idara ya Jiolojia kwa mwaka wa masomo 2014/2015. Udhamini huu utahusisha malipo ya gharama za ada, vitabu, pesa ya kijikimu na utafiti kwa muda wa miezi 18.
Katika hafla ya uzinduzi huu, Mgeni rasimi alikuwa Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Mizengo Kayanza Pinda. Wageni wengine walio alikwa na kufika ni Waheshimiwa Mabalozi wa nchi mbalimbali, akiwemo mkuu wa jumuia ya nchi za Ulaya, Wahadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar e salaam, viongozi wa makampuni ya gesi na mafuta na wa wakilishi kutoka taasisi mbalimbali za Serikali.
Ushiriki wa BG Tanzania unazingatia mpango mkakati wake wa muda mrefu wa kufanya kazi na kusaidiana na wadau mbalimbali ikiwa ni pamoja na taasisi za elimu ya juu katika kujenga uwezo na kuongeza utaalam kwa Watanzania kwenye shahada za juu za sayansi ya mafuta na gesi (MSc. in Petroleum Geology) lengo kuu ikiwa ni kuongeza fursa za ajira na utaalamu kwenye sekita za gesi na mafuta. Pia BG Tanzania, tangu mwaka 2012 imekuwa inatoa udhamini kwa ajili ya shahada ya juu vyuo vya nje na ndani ya nchi, hasa Uingereza. Wanafunzi 10 wamekuwa wanafaidika kupitia mpango huu kila mwaka.
Mkuu wa Kampuni ya BG ukanda wa Africa Mashariki, Ndugu, Derek Hudson, alisisitiza kuwa, mpango wa muda mrefu wa kampuni ya BG ni kufanya kazi na serikali pamoja na wadau wengine kuhakikisha watanzania wanahusika kikamilifu kwenye sekta ya nishati na gesi. Aliongeza kusema, BG Tanzania tunafurahi kuwa washirika na chuo kikuu cha Dar es salaam, hususani idara ya Geology. Ushirikiano wetu utajikita katika kujenga uwezo ili idara iwe na wataalam wakutosha kwa ajili ya kufundisha na kufanya tafiti mbalimbali za kisayansi.
Alisisitiza kwamba, ushirika huu wa BG na Chuo Kikuu cha Dar es salaam utadumu kwa muda wa miaka minne katika maeneo makuu matatu, (i) Udhamini wa wafanya kazi wa idara ya Geolojia kufanya shahada ya uzamivu (PhD) chuo cha Aberdeen - Uingereza, (ii) Udhamini wa wanafunzi 13, wanaofanya shahada ya uzamili ( MSc) elimu ya miamba na petrol ( Petroleum Geology) na kugharamikia wakufunzi ( Professors) kutoka chuo cha Aberdeen - Uingereza kuja kufundisha chuo kikuu cha Dar es salaam- idara ya Geology. Takribani dola milion mbili na nusu ($ 2.2m) zitatumika kwa muda wa miaka 4 katika utekelezaji wa hiyo miradi mitatu.
Katika hafla hii, Mh. Balozi wa serikali ya Uholanzi, akihutubia, alisisitiza ushirikiano endelevu wa sekta binafsi, hususani makampuni ya gesi na mafuta pamoja na chuo kikuu cha Dar es salaam.
BG Tanzania itaendelea kusaidia jitihada mbalimbali zinazohusiana na kujenga uwezo kwa taasisi na Watanzania kwa ujumla, hii itahusisha kuendelea kudhamini watanzania kufanya shada za juu ndani nan je ya nchi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...