BG Tanzania imetangaza  kutoa udhamini kwa wanafunzi 13 wa shahada ya uzamili  ya sayansi ya mafuta na gesi (MSc. in Petroleum Geology) itakayotolewa katika Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Idara ya  Jiolojia  kwa mwaka wa masomo 2014/2015. Udhamini huu utahusisha malipo ya gharama za ada,  vitabu, pesa ya kijikimu na utafiti kwa muda wa miezi 18.

Katika hafla ya  uzinduzi huu, Mgeni rasimi alikuwa  Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh.  Mizengo Kayanza Pinda. Wageni wengine walio alikwa na kufika ni Waheshimiwa Mabalozi wa nchi mbalimbali, akiwemo mkuu wa jumuia ya nchi za Ulaya,  Wahadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar e salaam, viongozi wa makampuni ya gesi na mafuta na wa wakilishi kutoka taasisi mbalimbali za Serikali.

Ushiriki wa BG Tanzania unazingatia mpango mkakati wake wa muda mrefu wa kufanya kazi na kusaidiana na wadau mbalimbali ikiwa ni pamoja na taasisi  za elimu ya juu katika kujenga uwezo na kuongeza utaalam kwa Watanzania kwenye shahada za juu za sayansi ya mafuta na gesi (MSc. in Petroleum Geology) lengo kuu ikiwa ni kuongeza fursa za ajira na utaalamu kwenye sekita za gesi na mafuta. Pia BG Tanzania, tangu mwaka 2012 imekuwa inatoa udhamini kwa ajili ya shahada ya juu vyuo vya nje na ndani ya nchi, hasa Uingereza. Wanafunzi 10 wamekuwa wanafaidika kupitia mpango huu kila mwaka.
Mkuu wa Kampuni ya BG ukanda wa Africa Mashariki,  Ndugu, Derek Hudson, alisisitiza kuwa, mpango wa muda mrefu wa kampuni ya BG ni  kufanya kazi na serikali  pamoja na wadau wengine kuhakikisha watanzania wanahusika kikamilifu kwenye  sekta ya nishati na gesi.   Aliongeza kusema, BG Tanzania tunafurahi kuwa washirika na chuo kikuu cha Dar es salaam, hususani idara ya Geology.   Ushirikiano wetu utajikita katika kujenga uwezo  ili idara iwe na wataalam wakutosha kwa ajili ya kufundisha na kufanya tafiti mbalimbali za kisayansi.
Alisisitiza kwamba, ushirika huu wa BG na Chuo Kikuu cha Dar es salaam utadumu kwa muda wa miaka minne katika maeneo  makuu matatu, (i) Udhamini wa wafanya kazi wa idara ya  Geolojia kufanya shahada ya uzamivu (PhD) chuo cha Aberdeen - Uingereza,  (ii) Udhamini wa wanafunzi 13, wanaofanya  shahada ya uzamili  ( MSc) elimu ya miamba na petrol ( Petroleum Geology) na  kugharamikia wakufunzi ( Professors) kutoka chuo cha Aberdeen -   Uingereza kuja kufundisha chuo kikuu cha Dar es salaam- idara  ya Geology.  Takribani dola milion mbili na nusu ($ 2.2m) zitatumika kwa muda wa miaka 4  katika  utekelezaji wa hiyo miradi mitatu.
​K​atika hafla hii, Mh. Balozi wa serikali ya Uholanzi, akihutubia,  alisisitiza ushirikiano endelevu wa sekta binafsi, hususani makampuni ya gesi na mafuta  pamoja na chuo kikuu cha Dar es salaam.
BG Tanzania itaendelea kusaidia jitihada mbalimbali zinazohusiana na kujenga uwezo kwa taasisi na Watanzania kwa ujumla, hii itahusisha kuendelea kudhamini watanzania kufanya  shada za juu ndani nan je ya nchi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...