Na Anitha Jonas – MAELEZO.
Taasisi ya Mwalimu Nyerere Foundation imeandaa mkutano wa mashauriano unaotarajia kufanyika tarehe Mei 19-20 mwaka huu, ambapo watajadili mambo mbalimbali kuhusu amani na utulivu wanchi ya Tanzania.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere Foundation Bw.Joseph Butiku alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kuhusu maandalizi ya mkutano huo na agenda za mkutano huo.
“Mkutano huu utahusisha viongozi wakuu wa Serikali ikiwemo walioko madarakani na waliokwisha kustaafu,viongozi wakuu wa Siasa na viongozi wa wakuu wa Dini na lengo kuu la kushirikisha viongozi hao ni kutafakari na kujadili hali ya amani,umoja,na utulivu wanchi yetu kwa kuzingatia kuwa viongozi hao ndiyo wenye jukumu na wajibu wa kwanza wa kusimamia amani na umoja”,alisema Bw.Butiku.
Mbali na hayo Bw.Butiku aliendelea kusema mkutano huo utajadili hoja mbalimbali ikiwemo masuala ya ukosefu ya ajira kwa vijana,kutoa ufafanuzi wa kuhusu Muungano,muongozo wa elimu kwa taifa letu pamoja na uanzishwaji wa vikundi vya ulinzi ndani ya vyama vya siasa.
Aidha hoja hizo ziliwasilishwa kwa wadau hao watakaoshiriki mkutano huo kwa ajili ya kutoa mapendekezo yao juu ya hoja hizo na zaidi ya washiriki kumi na nne wametoa mapendekezo yao katika hoja hizo na zitakazojadiliwa
.
Kwa upande mwingine Bw.Butiku alisema muasisi ya Mwalimu Nyerere Foundation Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alianzisha taasisi hiyo kwa lengo la kusimamia mwenendo wa amani na umoja kwa taifa na hivyo ndiyo maana wameandaa mkutano huo ilikujadili hatma ya taifa baada ya kuona uwepo kwa viashiria vinavyotishia amani na umoja.
Hata hivyo mkutano huo unatarajiwa kuwahudhiriwa na viongozi mbalimbali wakisiasa na wadini akiwemo Bw.Ibrahimu Lipumba (CUF),Bw.Wilbroad Slaa (CHADEMA),Bw.James Mbatia (NCCR) na Katibu wa Chama cha Mapinduzi Taifa Bw.Abraham Kinana,Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Bw.Philip Mangula,Katibu Mwenezi (CCM) Bw.Nape Nauye na viongozi wa dini ni uongozi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...