Ofisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Majisafi na Majitaka Dar es salaam (DAWASCO), Mhandisi Cyprian Luhemeja amesema kuwa katika uongozi wake mpya atasimamia maslahi ya wafanyakazi wa shirika hilo na kuwakomboa katika dimbwi la umaskini ili kuendana na mpango wa Matokeo makubwa sasa (BRN).

Ameyasema hayo jijini Dar es salaam katika kikao cha pamoja cha utambulisho wake kwa wafanyakazi wa Dawasco kilichowajumuisha wakurugenzi pamoja na wafanyakazi wa shirika hilo huku akisisitiza kuwa mshahara wa chini wa mwajiri katika shirika hilo utapanda ulipo hadi kufikia 650,000.

Ameahidi kuboresha hali ya upatikanaji wa Maji kwa maeneo sugu zaidi Dar ikiwa ni pamoja na kubuni miradi mipya na kusimamia miradi iliyopo ili kuongeza kasi ya makusanyo ya shirika na pia kuweza kulipa wafanyakazi maslahi mazuri zaidi.

“ongezeni kasi ya utoaji huduma kwa wateja na kuboresha mawasiliano na wateja kwani wao ndio kiungo muhimu katika kufikia malengo ya shirika na malengo yetu kwa ujumla” alisema Luhemeja Alisema katika uongozi wake atatengeneza DAWASCO mpya isiyo na fitina na itakuwa ni marufuku kwa watumishi wa shirika hilo kuitana wezi bila ya ushahidi na sababu za msingi, kufanya kazi kwa mazoea .

Luhemeja ni Afisa Mtendaji Mkuu aliyeteuliwa kuendesha shirika hilo kuanzia 01/05/2015 kwa mkataba wa miaka mitatu. Kabla ya kuja DAWASCO, Mhandisi Luhemeja alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Moshi (MUWSA).
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Majisafi na Majitaka Dar es salaam (DAWASCO), Mhandisi Cyprian Luhemeja akizungumza katika kikao cha pamoja cha utambulisho wake kwa wafanyakazi wa Dawasco kilichowajumuisha wakurugenzi pamoja na wafanyakazi wa shirika hilo, uliofanyika kwenye ukumbi wa JWTZ Kurasini jijini Dar
Sehemu ya Wfanyakazi wa Shirika la Majisafi na Majitaka Dar es salaam (DAWASCO) wakimsikiliza Ofisa Mtendaji Mkuu wao mpya, Mhandisi Cyprian Luhemeja (hayupo pichani).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...