Na Sultani Kipingo
Floyd Mayweather ameibuka mshindi katika pambano la karne baada ya kumdunda Manny Pacquiao kwa pointi nyingi alfajiri ya leo huko Las Vegas, Marekani.
Mmarekani Mayweather, 38, ametumia mbinu za hali ya juu za kujihami dhidi ya mpinzani wake Mfilipino, akifanya marekebisho muhimu kwenye raundi za awali kabla ya kupotea ulingoni.
Mayweather, ambaye ameongeza taji la WBO la uzito wa welterweight juu ya mataji ya WBC na WBA aliyonayo, alipewa ushindi kwa majaji watatu kuamua kapiga 118-110, 116-112 na 116-112.
Kwa ushindi huo, Mayweather amedhihirisha yeye ni bondia bora wa ngumi-kwa-ngumi wa zama hizi. Bingwa huyu anayeshikilia mataji matano sasa hajashindwa katika mapambano 48 katika miaka 19.
Akiwa bingwa wa mataji sita, Pacquiao, 36, anaishia ushindi wa mapambano 57, kapigwa mara sita na droo mbili.
Tiketi kwa mpambano huo wa karne ziliuzwa kwa dola £232,000 na mashabiki wa Marekani walicha dola 66 kuangalia kwenye luninga - kama ilivyokuwa duniani kote.
Na mshindi kwa pointi 118-110, 116-112 na 116-112... ni Mayweather!!! Floyd Mayweather alitamba ulingoni hadi dakika za mwisho... Floyd Mayweather akidunda Manny Pacquiao ![]() |
Floyd Mayweather |
Point 4 tu...acheni kupotosha habari.
ReplyDeleteSio point kibao uncle, ebu angalia 8, 4, 4 sema basi tu ila hatujui uenda kuna match fixing vile vile baada ya watu wengi kuweka mzigo maana mfilipino anao uwezo wa kumdunda jamaaa...
ReplyDeleteAaahahaah naona ankali kama umefurahi vile!! Yaani liver ww, Yanga ww hadi sasa naona upo team mayweather aahahhaah sipati picha!!
Mfilipino anatisha sana
ReplyDeleteMfilipino ingekuwa siyo bega ange mchapa jamaa
ReplyDelete