Na Mwandishi Maalum, New York 
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaamini kwamba, utekelezaji wa mipango na malengo ya mbalimbali ya maendeleo hayataweza kupatika au kufikiwa kwa haraka pasi na uwepo wa nishati endelevu na kwa wote. 
Ni kutokana na kulitambua hilo, Tanzania imejikita kikamilifu katika kukuza uwezeshaji wa matumizi ya teknolojia za kisasa na mbinu za kuongeza upatikanaji wa huduma za kisasa za nishati ikiwa ni pamoja na kuongeza maradufu kiwango cha uboreshaji na ufanisi wa nishati mbadala ili kuchagiza maendeleo. 
Hayo yameelezwa na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Mhe. Charles Kitwanga ( Mb), wakati akizungumza katika siku ya pili ya majadiliano ya mawaziri wanaohusika na sekta ya nishati ambapo kila waziri aliyehudhuria mkutano huo alipata fura ya kuelezea na kutoa ahadi ya namna inavyotekeleza mkakati wa nishati endelevu wa wote (SE4All). 
Mhe. Kitwanga na ujumbe wake unaowashirikisha wataalamu mbalimbali kutoka Wizara ya Nishati na Madini akiwano Kaimu Katibu Mkuu, Bw. Ngosi Mwihava wameshiriki kikamilifu katika mkutano huu ulioitishwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon, ambapo tangu ulipoanza mapema wiki hii, washiriki wamekuwa wakijadili mada mbali mbali zinazohusiana na masuala ya nishati, uwekezaji na mchango wake katika eneo zima la utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu. 
“ Tanzania inaamini kwamba hakuna ajenda za maendeleo zinazoweza kufikiwa kwa ukamilifu pasipo uwepo wa nishati ya uhakika” akasema Naibu Waziri Na kuongeza kuwa, mkakati wa nishati endelevu kwa wote ni nyezo muhimu katika kurahisisha ukusanyaji na uwekezaji wa raslimali inayohitajika ili kufika malengo ya kitaifa ya nishati endelevu kwa wote kufikia mwaka 2034 kama inayoainishwa katika mkakati huo. 
Kwa mujibu wa Naibu Waziri, Charles Kitwanga, Tanzania ilipitisha mkakati wa SE4All mwaka 2012 na kufuatiwa na mchakato wa kufanya tathmini ili kubaini mapungufu ambayo yalipelekea kutoa taarifa ya tathmini mwaka 2013. 
 Baada ya tathmini hiyo ilifuatia misaada kutoka SE4All kwaajili ya Afrika iliyosaidia kuandaa rasimu ya Ripoti na nchi ( Country Action Agenda) kwa ufadhili wa Banki ya Maendeleo ya Afrika, (AfDB) na Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Maendeleo ( UNDP). 
Kwa mujibu wa Mhe. Kitwanga, taarifa hiyo inatarajiwa kuwasilishwa kwa udhibitisho mwezi Agosti, 2015. Aidha maandalizi ya Mpango wa Uwezeshaji umeanza na utalenga katika kuangalia mahitaji ya haraka ili kuwezesha mpango huo kuanza kutekelezwa. Mkutano kuhusu Nishati Endelevu kwa wote (SE4All) umefungwa jana ( Alhamis).
 Mhe. Charles Kitwanga ( Mb) Naibu Waziri, Nishati na Madini akizungumzia namna  Tanzania  inavyotekeleza     Mkakati wa Nishati Endelevu kwa Wote  (SE4All) wakati wa  Mkutano wa siku Mbili wa  Mawaziri wa  Sekta ya Nishani,  uliofanyika  hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa.
 Wataalamu kutoka Wizara ya Nishati na Madini ambao wamefuatana na  Naibu  Waziri  katika mkutano huu muhimu  uliojadili kwa kina  nafasi na umuhimu wa nishati endelevu kwa  wote  katika kusukuma mbele malengo ya maendeleo endelevu , ukuaji wa uchumi, maendeleo ya jamii na utunzaji  wa mazingira.
 Kaimu Katibu Mkuu,  Bw. Ngosi Mwihava akiwasilisha  Action Agenda of Tanzania  kuhusu SE4All  katika moja ya mikutano  iliyofanyika hapa jijini  New York.
 Kaimu    Katibu Mkuu,  Bw. Ngosi  Mwihava akiwa  na wataalamu wake na wataalamu washauri  wakibadilishana mawazo kuhusu Action Plan of  Tanzania.
Mhe. Kitwanga akiteta jambo na  Mwakilishi wa  Bank ya Maendeleo  kwaajili ya Afrika  AfDB muda mfupi  mara baada ya   Naibu    Waziri kuzungumza ,  mkutano huu wa SE4All,  pamoja na  Mawaziri wa sekta husika umewashirikisha pia wadau mbalimbali wakiwamo wakuu wa  vyombo   vya fedha kama  vile Bank ya Dunia,  AfDB na wataalamu wengine wakiwamo pia wanamziki  maarufu ambao kwa namna moja ama nyingine wamekuwa wakichagiza na kuwekeza katika  nishati endelevu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...