MAULID
BARAKA KITENGE WITH CO HOST IBRAHIM
MASOUD “MAESTRO” NA OMAR KATANGA.
WACHAMBUZI
OSCAR OSCAR, MUSSA KAWAMBWA NA SUDI MKUMBA
WATAYARISHAJI
: YUSUPH MKULE, FRANCIS MHANDO, DR PANJUAN NA WENGINEO....
1.
MAULID
KITENGE NI NANI?,
Huyu ni mtangazaji nguli wa Sports Tanzania,
aliyetumia kipindi cha miaka kumi na nne(14) kwenye moja kati ya vituo maarufu
nchini Tanzania, na mwanzilishi wa Sports E FM Radio, ambae anafahamika sana
kwa utangazaji wake maridhawa, na maswali yenye kutia kashkashi ambayo huleta
mvuto mkubwa kwa wasikilizaji..na ambae anaamini kile anachokiamini yeye, na
akiwa ni mwenye kujiamini kwa mapana na marefu kitu kikubwa alichonacho Kitenge
ni hupenda kushauriwa na kumsikiliza kila mwenye kuhitaji kujifunza kutoka
kwake.
2.
IBRAHIM
“MAESTRO” MASOUD ..
Mtangazaji mwingine Nguli wa sports Tanzania, akiwa
muongozaji na mchambuzi mahiri wa sports kwenye Radio na Television, uzuri wa
huyu bwana aliwahi kuwa mchezaji wa klabu kadhaa za ligi mbalimbali Tanzania
bara na Visiwani, na ambae pia ni mwalimu wa soka wa Ngazi ya kati, na mwenye
taaluma ya soka la vijana aliyebobea, akiwa nauzoefu wa miaka isiyopungua kumi
na minne (14) kwenye kiwanda cha habari za michezo Tanzania...
3.
OMARY
KATANGA…
Mtayarishaji na muongozaji pia muanzilishi wa
E-Sports ya E-fm mbali na umahili wake katika sports, lakini pia ni msomaji
mzuri wa Taarifa za habari, anatumia
style ya kipekee inayopendwa na wasikilizaji ya kwenda speed wakati wa kutangaza michezo, ana maswali ya mtego yenye kuleta
burudani masikioni mwa wasikilizaji wakati akifanya mahojiano na watu waliomo
kwenye familia ya michezo, ni mtangazaji makini sana kwa kila akipelekacho
hewani.
4.
OSCAR
OSCAR..
Kitaaluma ni mwalimu, na ambae ameibuka kuwa mmoja
kati ya wachambuzi wanaokuja juu sana kwenye michezo Tanzania kutokana na kuwa
mfuatiliaji sana wa masuala ya soka, na
mara nyingine hufanya uchambuzi kwenye
vipindi vya TV kama Kabumbu show, na uchambuzi wa mechi za Premier ya England,
kwenye kituo cha Utangazaji cha
Kimataifa-BBC.
5.
MUSSA
KAWAMBWA..
Ni mchambuzi na muaandaji wa kipindi cha michezo
hapa 93.7 EFM mwenye uzoefu wa hali ya juu katika tasnia hii akiwa amepita
katika vituo mbalimbali vikubwa hapa nchini, pia ni muandaaji wa kipengele cha
HISABATI ndani ya Sports Headquarters na Chakuchabo. Sauti yake ya kuvutia
pamoja na historia kubwa aliyonayo hasa katika soka la barani Ulaya ni moja
kati ya vitu vinavyomfanya awe wa kipekee. Mwisho kabisa ni uelewa wake juu ya
michezo kama Tennis, Cricket, Rugby, Masumbwi na Langalanga.
1.
FRANCIS
MUHANDO.
Ni mtayarishaji na reporter wa vipindi vya michezo hapa 93.7 EFM,
unayeweza kumsikia katika kipengele cha Robo saa ya nguvu akifanya mahojiano na
wanamichezo mbalimbali.
2.
YUSUPH
MKULE.
Mtayarishaji na muongozaji wa vipindi vya michezo
hapa Efm, E.Sports & Sports HQ na amekuwa mtangazaji wa michezo tangu mwaka
2009 kwakufanya kazi katika redio mbalimbali hapa nchini Tanzania. Pia amewahi kuwa msimamizi
wa vipindi katika mmoja ya redio aliyowahi kufanya kazi katika mikoa ya nyanda
za juu kusini mwa Tanzania.
Kwaujumla ni kati ya watangazaji na waongozaji wa
vipindi vya michezo ambaye kwasiku za usoni atakuwa moto wa kuotea mbali
na hilo analithibitisha katika kipinchi cha E.Sports na Sports HQ hapa E.FM.
3.
SUDI
MKUMBA.
Mtayaarishaji na mchambuzi wa vipindi vya E Sports na Sports HQ ni ni miongoni mwa
walioanzisha vipindi hivi vya michezo
hapa 93.7 EFM pia ndiye mchambuzi wa kipengele cha michezo katika kipindi cha
UBAONI kinachoongozwa na mtangazaji Gadner G Habash.
Ni mchambuzi anaechipukia na anaekuja kwa kasi kubwa
katika tasnia hii ya uchambuzi na uandaaji wa vipindi vya michezo radioni.
SPORTS
HEADQUATERS..
Ni show ambayo imekusanya michezo yote duniani,
ambayo Platfom yake ni E Sports, ikiwa na Vipengele mbalimbali kama vile habari
za nyumbani na uchambuzi yakinifu, Robo saa ya nguvu ya kwanza ambayo
inahusisha mahojiano ya wanamichezo mbalimbali, Hisabati, Maswali ya Dr
Panjuani, Robo saa ya pili ya nguvu kwa habari za kimataifa, ikiwemo Soka,
Basketball, Boxing,Tennis, Rugby,Formula 1,Golf, Cricket, Netball na kadhalika,
na mwisho kuna kitu kinaitwa, Cha kuchabo,,ambacho kinapekua habari
zilizojificha.
Pamoja na yote hayo, bado pia kuna burudani ya
kutosha ua muziki uliopangika vizuri toka kwa ma Dj waliobobea kwenye Burudani,
RDJ’S.
MKUU HII IMETULIA SANA!! UNAWEZA KUWEKA PICHA ZAO/PICHA ZA MUHUSIKA JUU YA KILA MAELEZO YAKE CHINI YA JINA LAKE ...Tupate kuwajua watu hawa Mahiri!!! Asanteni sana efm kwa mapinduzi makubwa mliyoleta
ReplyDeleteThat what you call all stars AKA dream team,what a combination?kudos to efm management keep good work.
ReplyDelete