Hivi ndivyo hali ilivyo katika hili ni Daraja lilalounganisha eneo la Tandale na Mwananyamala jijini Dar es Salaam, ambapo wananchi wanaokaa maeneo ya jirani na Daraja hilo waliamua kukusanya viroba vilivyosheheni taka ngumu na kuwevilundika kwenye kingo za Daraja hilo ili kudhibiti maji yasiendelee kuchimba njia hiyo. Hali hii imekuja kutokana na mafuriko ya maji yaliyotokea hivi karibuni katika maeneo mengi hapa jijini kutokana na Mvua kubwa zilizokuwa zikinyesha.

Hali ilivyo katika mfereji unaopitisha maji katika eneo hilo baada ya kupitiwa na Mafuriko hivi karibuni.
Oooohhh no, is this real? I can't imagine how someone can actually live near that mfereji? It is dangerous in all aspects.
ReplyDeleteUmaskini una shida
ReplyDeleteNa iwe hivyo, mlivyoambiwa msichimbe mchanga kwenye madaraja mliweka pamba masikioni! Hayo ndio matokeo ya ubishi wenu. Ona madaraja mengine kama lugalo, mbezi,kijichi,goba.....watu wanaendelea kuchimba mchanga kama serikali haipo.
ReplyDeletesasa hapa diamond ndo angekazia msaada wake aokoe eneo alilokulia au sio.
ReplyDeleteMiji mingine kandoni mwa maji kama haya unakuta miti na maua na viti kwa watu kupumzikia!! Hapa ni magonjwa tu utapata!!
ReplyDeleteKweli tumeshindwa kujitawala!!
Hakuna Mipango hapo, wananchi wanaoishi hapo ni wachafu na serikali pia ya eneohilo/mtaa/kijiji/kata/wilaya/mkoa nayo inaendekeza uchafu. Baada ya 5yrs hapo wasipo chukua hatua maji yatatuama na takataka zitaingia mpaka majumbani kwao. AIBU.
ReplyDelete