![]() |
DENNIS SSEBO NA ADELLA TILLYA.
|
1. 12:00
HADI SAA 3:00 KAMILI ASUBUHI UNAPATA
" JOTO LA ASUBUHI" ILI KUKUANZISHIA SIKU
" JOTO LA ASUBUHI" ILI KUKUANZISHIA SIKU
DENNIS
SSEBO NI NANI?
Ssebo ni moto
ama baruti ya kipekee katika masuala ya Radio, akiwa ni muhitimu wa mambo ya
sheria na ana shahada ya udhamiri katika
mambo ya mawasiliano ya Umma lakini akiwa na ufahamu na mapenzi zaidi upande wa Radio na TV.
Ssebo amekuwa kwenye Tasnia hii kwa muda mrefu akiwa
na uzoefu wa kufanya kazi Zaidi Radio na
Tv kwa muda wa miaka 15, lakini pia amekuwa akisaidia kwakiwango kikubwa sana
katika kuboreha vipindi vya Radio na Tv
nchini Tanzania.
Wapo watu wachache ambao wanatambua uwezo wake
wakuburudisha na kufundisha, Zaidi
amejulikana kuwa ni mtu wa masihala au utani lakini Dennis Ssebo ni mtu makini
anayejitambua na muda wake mwingi ameutolea kwenye kusoma na kufanya tafiti
mbalimbali.
Ssebo anasema “ Ninasema kile ambacho ninakiona,
lakini kama hukubaliani nacho ni uamzi wako”
Mpende au umchukie lakini kwa hakika utacheka, utashangaa na utajifunza
kitu unapomsikiliza radioni.
Ssebo ni mtangazaji ambaye EFM Radio imempa nafasi
ya kukuamsha na kuwa nawe kila siku asubuhi
kuanzia saa kumi na mbili hadi saa tatu kamili asubuhi , Jumatatu hadi
ijumaa.
MJUE ADELLA TILLYA
MJUE ADELLA TILLYA
Na hiyo sauti ya kike unayoisikia kila siku pamoja
naye asubuhi, si ya mwingine bali ni mwanadada
shupavu ( Iron Lady) ambaye huwezi kumpata sehemu yoyote Zaidi ya Efm
Radio.
Hapa namzungumzia Adella Tillya, ambaye ni mtayarishaji wa Kipindi cha Joto la Asubuhi na
juhudi zake mara nyingi zinatambuliwa sana na Ssebo ambaye amekuwa
akimwambia “ katika wewe ninaona
taarifa”
Adella amekuwa na uzoefu wa kuandaa na
kutangaza na ni miongoni mwa watangazaji
wa chache ambao mpaka sasa wameweza kumshika Ssebo.
Ni ajabu hata katika ofisi za Efm amekuwa akiitwa
mwanamke shupavu na hata akisikika hewani
akicheka lakini haimanishi kuwa ni mwanamke wa kawaida.
Ni watu hawa wawili, watundu,
lakini wakiwa na taarifa za kutosha za mambo mbalimbali ambao kwa pamoja
wanakupa Joto la Asubuhi.
Katika kipindi cha Joto la Asubuhi, utapata habari za ndani na Nje ya nchi, uchambuzi wa
magazeti ya ndani na nje, mada mbalimbalimba kuhusiana na mambo yanayoendelea
ulimwenguni bila kusahau zawadi zitolewazo kwa wasikilizaji.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...