Naibu waziri wa kazi na ajira, Mheshimiwa Makongoro Mahanga akimkabidhi cheti cha kutambua mchango wa serikali ya Zanzibar katika mradi wa ujasiriamali, ndugu Ameir Ali Ameir, ambaye ndiye Mkurugenzi wa Ajira kutoka Ofisi ya Rais Kazi na Utumishi wa Umma, Zanzibar.
Naibu waziri wa kazi na ajira, Mheshimiwa Makongoro Mahanga akizungumza na waandishi wa habari.
 Mkurugenzi Mkazi wa UNDP, Philippe Poinsot akizungumza wakati wa kongamano.
 Mkurugenzi Mkuu wa ILO Tanzania, Kenya, Uganda na Rwanda Bwana Alexio Musindo akizungumza na waandishi wa habari.
   Baadhi ya wahudhuriaji wa kongamano la kuadhimisha Miaka mitano ya mradi wa Ujasiriamali uliokuwa unaendeshwa na Shirika la Kazi la Kimataifa (ILO).

ILO Tanzania yaadhimisha miaka 5 ya kuwawezesha vijana Tanzania kupitia ujasiriamali. Shirika la Kazi la Kimataifa (ILO) leo limeadhimisha miaka 5 toka kuanzishwa kwa mfuko wa ujasiriamali wa vijana (YEF) kwa kuandaa kongamano katika ukumbi wa Mwalimu Julius Nyerere.

Mfuko wa Ujasiriamali kwa vijana ulizinduliwa mwaka 2010 ukilenga katika kutengeneza ajira kwa vijana kwa kupitia ukuzaji wa sekta binafsi pamoja na kuongeza ushindani kwenye uchumi wa Afrika.

Mradi ulijikita katika kuwatengenezea vijana ajira nzuri, kukuza ujasiriamali na kuwatengenezea fursa vijana wa kiafrika kupitia elimu, kuwaongezea ujuzi na uwezeshaji wa mtaji. Kwa kupitia mradi huu wa Kuwezesha Ujasiriamali, Mfuko wa Ujasiriamali kwa vijana ulilenga kutengeneza maelfu ya ajira kwa vijana katika nchi za Kenya, Tanzania na Uganda.

Msingi mkuu wa mradi ulikuwa kukuza utamaduni wa ujasiriamali miongoni mwa vijana, kuingiza elimu ya ujasiriamali katika mitaala, kuongeza uwingi wa mambo yanayowezekana katika ajira kwa vijana, kuwezesha taasisi za vijana kutekeleza mawazo mazuri ya ujasiriamali na kuwezesha upatikanaji wa mitaji kwa vijana walio nje ya shule.

Toka mradi umeanzishwa, umewezesha zaidi ya vijana 30,000 ambao ni wajasiamarali wapya na waliopo kupitia utoaji wa elimu ya biashara, kusaidia uanzishwaji wa biashara zaidi ya 17,000 pamoja na utengenezaji wa zaidi ya ajira 40,000 kwa vijana, ambayo vyote kwa pamoja vimevuka malengo ya mradi yaliyoaninishwa mwanzo.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...