Jamuhuri ya Kiislamu ya Iran ina wajibu wa kuendelea kuiunga mkono Zanzibar katika harakati za maendeleo kutokana na Historia ndefu iliyopo ya mwingiliano wa kibiashara baina ya baadhi ya Wananchi wa pande hizo mbili.
Gavana Mkuu wa Jimbo la Sistan na Balachestan Nchini Jamuhuri ya Kiislamu ya Iran Bwana Ali Osat Hashemi akiuongoza Ujumbe wa Viongozi saba wa Jimbo hilo alieleza hayo wakati akizungumza na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.
Gavana Ali Osat Hashemi alisema muingiliano huo wa biashara kati ya Irani na Zanzibar na Tanzania kwa ujumla umepelekea watu wa pande hizo mbili pia kuwa karibu zaidi kwa kuchanganya damu.
Alisema wiki chache zijazo pande hizi mbili zinatarajia kusaini Mkataba wa ushirikiano katika kuendeleza mradi wa mafunzo ya amali ambao utagharimiwa na Iran kwa kiasi cha Dola za Kimarekani Laki 500,000 zitakazotumika katika ununuzi wa vifaa vya kufundishia.
Gavana huyo wa Jimbo la Sistan na Balachestan Nchini Jamuhuri ya Kiislamu ya Iran alifahamisha kwamba sekta binafsi hasa miradi ya amali inafaa kuungwa mkono kwa vile inasaidia kutoa ajira kubwa kwa Jamii hasa Vijana.
Akitoa shukrani zake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema miradi ya Amali na Sekta ya Afya inayofadhiliwa na Iran kwa Zanzibar ni uthibitisho wa uimarishaji wa uhusiano uliopo kati ya pande hizo mbili.
Wakati huo huo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alikutana kwa mazungumzo na Balozi Mpya wa Malawi Nchini Tanzania Bibi Hawa O.
Ndilole aliyefika kujitambulisha rasmi Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.
Akizungumza na Balozi Mpya wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Nchini Japani Balozi Batilda Buriani aliyefika Ofisini kwake Vuga kumuaga rasmi baada ya kuteuliwa kushika wadhifa huo Balozi Seif alimuomba Balozi Batilda kuhakikisha kwamba Tanzania inafaidika kutokana na ushirikiano wake wa Kidiplomasia ya Japan.
Balozi Mpya wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Nchini Japan Balozi Batilda Buriani akisalimiana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alipofika kuaga rasmi baada ya kuteuliwa kushika wadhifa huo na Rais wa Jakaya Mrisho Kikwete.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akimkaribisha Balozi Mpya wa Malawi Nchini Tanzania Bibi Hawa Ndolowe aliyefika Ofisini kwake kujitambulisha rasmi.
Balozi Seif akisalimiana na Gavana Mkuu wa Jimbo la Siustan na Balachestan Nchini Jamuhuri ya Kiislamu ya Iran Bwana Ali Osat Hashemi wakati alipofika na ujumbe wake kwa mazungumzo ya uhusiano kati ya nchi hizo mbili.
Balozi Seif akibadilishana mawazo na Gavana Mkuu wa Jimbo la Siustan na Balachestan Nchini Jamuhuri ya Kiislamu ya Iran Bwana Ali Osat Hashemi ambae yupo Zanzibar na Ujumbe wake kwa ziara ya siku mbili.
Picha na OMPR – ZNZ.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...