Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua
Bwana Anthony Peter Mavunde kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa, Mkoa wa Dodoma,
kuanzia leo, Jumatatu, Mei 25, 2015.
Aidha,
Rais Kikwete amefanya uhamisho wa wakuu 10 wa Wilaya kwa nia ya kuongeza
ufanisi katika uongozi wa Wilaya mbali mbali nchini.
Katika
mabadiliko hayo, Rais Kikwete amemhamisha Luteni Edward Ole Lenga kutoka Wilaya
ya Mkalama, Mkoa wa Singida kwenda kuwa mkuu wa wilaya mpya ya Kyerwa, Mkoa wa
Kagera. Luteni Lenga anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Luteni Kanali Benedict
Kulikela Kitenga ambaye alifariki dunia Aprili 20, mwaka huu, 2015.
Wakuu
wengine wa wilaya ambao Rais Kikwete amewahamisha ni Elizabeth Chalamila Mkwasa
kutoka Wilaya ya Dodoma kwenda Wilaya ya Mvomero, Mkoa wa Morogoro, Dkt.
Jasmine Tisike kutoka Wilaya ya Mpwapwa kwenda Wilaya ya Dodoma, Agnes Elias
Hokororo kutoka Wilaya ya Namtumbo, Mkoa wa Ruvuma kwenda Wilaya ya Tunduru,
mkoani humo humo na Fadhili Nkurlu kutoka Wilaya ya Misenyi, Mkoa wa Kagera
kwenda Wilaya ya Mkalama.
Wengine
ambao wamehamishwa ni Chande Bakari Nalicho kutoka Wilaya ya Tunduru kwenda
Wilaya ya Namtumbo, Festo Shem Kiswaga kutoka Wilaya ya Mvomero kwenda Misenyi,
Darry Ibrahim Rwegasira kutoka Wilaya ya Karagwe, Mkoa wa Kagera kwenda Wilaya
ya Biharamulo, mkoani humo humo, Elias Choro John Tarimo kutoka Wilaya ya
Biharamulo kwenda Chunya, Mkoa wa Mbeya na Deodatus Lukas Kinawiro kutoka
Wilaya ya Chunya kwenda Wilaya ya Karagwe, Mkoa wa Kagera.
Imetolewa
na;
Kurugenzi
ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es
Salaam.
25
Mei, 2015
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...