Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya mikopo ya nyumba ya Tanzania Mortgage Refinance (TMRC), Oscar Mgaya (kulia) akipokea jijini Dar es Salaam,  mfano wa hundi ya Dola za Kimarekani milioni moja kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya SHELTER AFRIQUE, James Mugerwa (wa pili kushoto), baada ya kampuni hiyo kununua hisa asilimia 11.6 katika TMRC. Wengine kutoka kushoto ni Ofisa Fedha Mkuu wa TMRC, Oswald Urassa na  Mkurugenzi wa Uendeshaji na Mfumo Habari wa taasisi hiyo, Shabani Mande.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya mikopo ya nyumba ya Tanzania Mortgage Refinance (TMRC), Oscar Mgaya (kulia) akibadilishana mawazo na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya SHELTER AFRIQUE, James Mugerwa (katikati) na Ofisa Fedha Mkuu wa TMRC, Oswald Urassa (kushoto) katika hafla hiyo. Taasisi ya TMRC ina wanahisa 14 ambao ni benki za Exim, NMB, CRDB, NBC, Azania, TIB, DCB, NIC, ABC, PBZ, BOA, I&M Bank, NHC na SHELTER AFRIQUE.  
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya mikopo ya nyumba ya Tanzania Mortgage Refinance (TMRC), Oscar Mgaya (wa sita kushoto) akizungumza kabla hajapokea  mfano wa hundi ya Dola za Kimarekani milioni moja kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya SHELTER AFRIQUE, James Mugerwa (kulia kwake), baada ya kampuni hiyo kununua hisa asilimia 11.6 katika TMRC. Wengine ni maofisa wa TMRC.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...