Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda akiwa katika majadiliano na Maafisa wa Jeshi la Polisi juu ya namna ya kuumaliza mgomo wa Madereva wa Mabasi katika stendi kuu ya Ubungo, Jijini Dar es salaam leo. Hapo wanasubiriwa viongozi wa Madereva hao.
Hali ilivyo Stendi Kuu ya Mabasi, Ubungo jijini Dar hivi sasa. hakuna basi lililoweza kuondoka siku ya leo.
Kikao cha nje kikiendelea.
 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda (kushoto) akiambatana na Kamanda wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, DCP Mohamed Mpinga pamoja na maafisa wengine wa Jeshi la Polisi walielekea zilipo ofisi za Umoja wa Madereva, Ubungo jijini Dar es salaam ili kwenda kuzungumza nao juu ya mustakabali wa Mgomo wao huo.
Serikali ikisikiliza kwa makini matakwa ya Madereva hao.
Kina Ras Makunja wakiwa wametulia garini kuhakikisha usalama unapatikana katika eneo hilo
Hakufanyiki kitu Ubungo leo, ni shangwe kwa kwenda mbele kwa Madereva hao pamoja na utingo wao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 05, 2015

    Madereva watoe huduma wakati mambo yao yanashughulikiwa, kwa nini watu waumie watembee wengine wanataka kuwahi kwa ajili ya matibabu, wengine wanaenda mikutano, wengine wanarudi makwa baada ya biashara, wapo wanaouguza au wanahitaji kufika sehemu fulani kushughulikia mambo yao mnapo wakwamisha hamuikomoi serikali mnatuumiza sisi wananchi wa kawaida wateja wenu. Kumbuka mnatoa huduma, sekata hii zamani ilikuwa na mabasi ya serikali sasa hivi mmeachiwa watu binafsi. HAYA MAMBO YA KUUMIZA WANANCHI KUTEMBEA SIYO MAZURI. TOENI HUDUMA MATATIZO YENU YATASHUGHULIKIWA

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 05, 2015

    Hapo Kina Ras Makunja wanasubiri amri muziki uanze,magitaa yote wanayo

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 05, 2015

    kina ras makunja wapo gado! jamaa awapendagi mazungumozo mengi watu wakileta za kuleta wao wanapiga muziki

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 05, 2015

    naona wagaga gigikoko kina ras makunja wamekaa mkao wa kula

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 05, 2015

    kina Ras makunja wakiwa tayari tayari kuanza muziki wanasubiri washabiki waanze kushangilia

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 05, 2015

    Kama kuna watendaji wanaosababisha kero kwa madereva wapokee ujumbe waache tabia hizo au wajue kama wakiendelea wawajibishwe.

    ReplyDelete
  7. Kwhyo raia aendelee kuteseka, maana ana thamani gani, kma wenyewe wana magari yao

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 05, 2015

    Ila Dar nako kuchafu jamani kweli hali hii mpaka leo 2015 bado miundombinu hovyohovyo, da! ni aibu sana. Yaani ni walau jiji kubwa lingekuwa hata Mwanza au Arusha kuliko Dar. Ni mji mchafu sijapata kuona Duniani lol!

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 06, 2015

    Kuchafu kweli, inaelekea sisi watu weusi uchafu ni kama rafiki zetu,kunatia hata aibu, eti ndio mji mashuhuri wa Tanzania, na hapo eti ndio stendi kubwa ya Tanzania,hmmm na sura za umasikni etii

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...