Mahakama ya Umoja wa Mataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (UN-ICTR) imetoa msaada wa gari lililoimarishwa kiusalama - amored vehicle - linaloonekana nyuma kwa Idara ya Magereza nchini kwenye sherehe fupi iliyofanyika mjini Arusha. Akikabidhi gari hilo Mkugenzi wa Idara ya Utawala wa ICTR Dr. Saraha Kilemi alisema kuwa msaada huo ni shukrani za mahakama hiyo kwa Idara hiyo kwa ushirikiano iliyoutoa kwa mahakama hiyo kwa kipindi cha miaka zaidi ya 20 ya kazi za mahakama hiyo nchini. 
Akipokea msaada huo Naibu Kamishna Mwandamizi  wa Magereza Bw. Hamis Nkubasi aliishukuru mahakama hiyo akiongeza kuwa hilo ni gari la pili kutolewa na ICTR  kwa Magereza. Gari la kwanza limeshahamishiwa Dar es Salaam. Gari lingine la tatu aina hiyo liliwahi kutolewa na ICTR kama msaada miezi michache iliyopita kwa Ofisi ya Waziri Mkuu kupitia Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Pichani Dr. Kilemi (wa tatu kushoto) akikabidhi funguo za gari hilo kwa Bw. Nkubasi (wa nne kulia). Wakishuhudia ni maofisa wa Magereza na ICTR  wakiwamo Afisa Habari wa ICTR Bw. Danford Mpumilwa (wa kwanza kushoto), Mkuu wa Usalama na Ulinzi wa ICTR Bw. Saidou Giindo (wa pili kushoto) na Bw. Jerry Mburi, Afisa Sheria wa ICTR (wa kwanza kulia) 
 Afisa Magereza akisaini kupokea gari hilo 

  Gari  lililoimarishwa kiusalama - amored vehicle iliyokabidhiwa na  Mahakama ya Umoja wa Mataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (UN-ICTR) kwa Magereza nchini kwenye sherehe fupi iliyofanyika mjini Arusha.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...