1.USHAHIDI  WA  KUAMBIWA  NI NINI?
Ushahidi  wa  kuambiwa  ni  ushahidi  unaotolewa  na  mtu  ambaye  hakuona  tukio  likitendeka,  hakusikia  tukio  likitendeka,  hakuhisi  wala  kuonja,  wala  kunusa  jambo  lililo mbele  ya  mahakama  kama  kosa  isipokuwa   aliambiwa    na  mtu  mwingine aliyeona,  kusikia, kuhisi, kunusa  au  kuonja.  
Hapa  kuna  watu  wawili,  kwanza  aliyeona au kusikia , na  pili  yule  aliyeambiwa  na  huyu   aliyeona   au  kusikia .   Kwahiyo   katika maana  yetu    huyu   wa  pili  aliyeambiwa  na  wa  kwanza  aliyeona  au  kusikia   ndiye  mwenye  ushahidi  wa  kuambiwa.  Ni  kwa  maana  hii tunasema  huyu  wa  pili  aliyeambiwa  akienda  kutoa  ushahidi  wake  mahakamani    utaitwa  ushahidi  wa  kuambiwa.


Kwa  mfano  “A”  amemuona “ B”  akimuua  “C”.  “ A”  baada  ya  kuona  tukio  lile  akamwambia  rafiki  yake  “D”.  Ina  maana  “D”  hakuona  lolote  isipokuwa  ameambiwa  na  rafiki  yake  “A”  aliyeona. Kwa  maana  hii  ushahidi  wa  “D” ni  ushahidi  wa  kuambiwa.  Ameambiwa  na  nani,  ameambiwa  na  “A”  aliyeona  tukio.  Hii  ndio  maana  ya  ushahidi  wa  kuambiwa.  Kwa  jina  la  kitaalam  ushahidi  huu  huitwa “hearsay  evidence” .  Na  kwa  jina  jingine  la  mtaani  huitwa “ ushahidi  wa  nilimsikia  akisema”. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...