Na Bashir Yakub.
Kutokana na maendeleo ya biashara duniani kote imekuwa ni vigumu sasa kufanya biashara nje ya kampuni. Hii ni kwasababu kila kampuni au taasisi utakayotaka kufanya nayo biashara iwe kununua kwao au kuuza kwao basi kitu cha kwanza watakachokwambia ni kuwa hatufanyi biashara na watu binafsi.
Zipo biashara ambazo watu wengi bado wanazifanya nje ya kampuni lakini ukweli ni kuwa biashara hizo kwa ulimwengu wa biashara wa sasa ni za kienyeji na tija yake bila shaka ni ya kusuasua.
Kwa hali ilivyo sasa hadi migahawani unaposupply mayai au kuku wa nyama n.k sio muda mrefu watakwambia sasa tunahitaji kampuni ndio isupply na sio mtu binafsi . Kama hali ni hiyo nini basi mjasiriamali wa leo afanye.
1.NINI MJASIRIAMALI AFANYE KWA SASA.
Kilio cha mjasiriamali makini siku zote huwa hali na wala halali isipokuwa anawaza nini kesho afanye ili biashara zake zitoke hapo zilipo na kwenda hatua nyingine mbele. Mjasiriamali mwenye mawazo hayo ndiye huanza na mtaji wa elfu kumi baada ya mwaka zikazaa milioni tano na baada ya miaka akamiliki milioni mia. Huyu huitwa mjasiriamali mwenye fikra chanya( positive thinking enterprenuer) . Nimesema hapo juu kuwa hali ya biashara imebadilika kwa namna ambayo wadau wa biashara wamejielekeza katika kufanya kazi na makampuni badala ya watu binafsi kama tulivyozoea.
Swali la nini mjasiriamali afanye katika hali hiyo jibu lake ni kuwa mjasiriamali naye abadilike. Kama mwaka jana ulifuga kuku wewe kama wewe binafsi basi leo fuga kuku chini ya kampuni, kama mwaka jana ulilima mihogo Chanika na kuuza sokoni wewe kama wewe basi leo lima mihogo na uza lakini si kama wewe binafsi isipokuwa chini ya kampuni. Una tigo pesa yako, duka, liwe la mavazi au bidhaa nyingine, fundi fenicha, unamiliki taxi, fundi cherehani, na kila kitu unachofanya kwa ajili ya kipato basi sasa ni wakati kumiliki kitu hicho kupitia kampuni.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...