Huwezi kufikiria umiliki wa kampuni kabla ya kufikiria kuhusu mtaji wa kampuni. Mtaji wa kampuni ni suala nyeti kwa wenye wazo la kumiliki kampuni au wanaomiliki kampuni tayari. Mtaji ndio kila kitu katika kampuni. Tangu unapokuwa katika harakati za kusajili kampuni utalisikia neno hili mtaji karibia katika kila hatua unayopita. Niseme mapema kuwa mtaji mdogo ndio kampuni ndogo na mtaji mkubwa ndio kampuni kubwa. Kwa hili mitaji imegawanyika mara mbili upo mtaji wa maandishi unaokuwa kwenye katiba na waraka wa kampuni( MEMAT) na upo mtaji wa mali halisi ( physical assets).
Mtaji wa unaokuwa kwenye nyaraka nilizotaja mara nyingi hautambulishi ukubwa au udogo wa kampuni. Hii ni kwasababu mtaji huu huwa ni maandishi tu na yawezekana kiwango cha fedha kilichoandikwa humo kama mtaji hakipo kabisa katika kampuni. Hivyo mtaji wa aina hii hauna uhusiano wowote na ukubwa au udogo wa kampuni. Kwa upande wa mtaji wa mali halisi huu ndio mtaji ambao huweza kutambulisha ukubwa au udogo wa kampuni. Hii ni kwasababu mtaji huu huwa sio maneno tu au maandishi bali mali kwa maana ya mali . Na kisheria mali kama mali za kampuni ndio mtaji wa kampuni na ndio nitakaozungumzia hapa. Nitazungumzia mtaji lakini zaidi ni kujua mtaji hujumuisha nini.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...