Na Bashir Yakub.
Mara nyingi nimeandika kuhusu ardhi hususan viwanja na nyumba. Katika kufanya hivyo mara kadhaa nimejaribu kuwatahadharisha watu namna mbalimbali ya kisheria ya kuepuka kuingia katika migogoro ya viwanja na nyumba hasa wakati wa kununua( wanunuzi).
Nimewahi kueleza namna au vitu vya msingi ambavyo hutakiwa kuwa katika mkataba wa ununuzi wa nyumba au kiwanja. Nikaeleza umuhimu wa kila kimoja na nikasisitiza kuwa atayekuwa amenunua ardhi na mkataba wake ukajaaliwa kuwa na vitu hivyo basi si tu atakuwa amefanya manunuzi bora lakini pia atakuwa amefanya manunuzi yanayokubalika kisheria.
Ifike hatua watu waelewe kuwa migogoro mingi ya ardhi huanzia na kutokuwa makini kwenye manunuzi. Kutokupata ushauri wa kisheria ikiwa ni pamoja na kutopitia hatua za msingi za kisheria kabla ya manunuzi, kuandikiwa mikataba ya manunuzi isiyokidhi vigezo vya kisheria ikiwemo ile ya serikali za mitaa ambayo hairuhusiwi kabisa kisheria ni kati ya sababu chache kati ya nyingi zitakazokupelekea uingie katika mgogoro. Leo nitaeleza hatua moja ya msingi sana ambayo hutakiwi ufanye manunuzi ya ardhi bila kuipitia.
1.HATUA TANO ZA KUFUATA UNUNUAPO NYUMBA/KIWANJA.
Ziko hatua tano muhimu za kupitia pale unapo kuwa katika mchakato wa kununua ardhi. Umuhimu wa hatua hizi ni kuwa kwanza kabisa si rahisi kujikuta katika mgogoro unapokuwa umezipitia. Lakini pili hata bahati mbaya utokee mgogoro basi wewe uliyepitia hatua hizo utakuwa salama na kama ni kesi basi wewe upo katika mazingira mazuri ya kushinda. Hatua ya kwanza huitwa hatua kabla ya mkataba( pre contractual stage).
Hatua hii inayo mambo yake ya msingi na ya kisheria ambayo kuyafuata kwako kwaweza kukuweka mbali na hatari ya kununua ardhi yenye mgogoro au itayokuingiza katika mgogoro . Hatua hii ndiyo nitakayoeleza kama msingi wa makala ya leo kama tutakavyoona. Kabla ya kueleza hatua hiyo ni vema pia nikazitaja hatua nyingine japo kwa ufupi. Hatua ya pili huitwa hatua ya mkataba( contractual stage). Hii ni hatua ya kupitia na kujiridhisha na mkataba wa manunuzi ikiwa ni pamoja na kuusaini. Hatua ya tatu huitwa “pre completion stage”, hatua ya nne huitwa hatua ya kumalizia ( completion stage) na hatua ya tano na ya mwisho huitwa hatua baada ya kumalizia ( post completion stage).
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...