Na Bashir Yakub.
Mara nyingi unapounda kampuni huwa ni lazima kueleza katika zile Memorandum kuhusu ukurugenzi na wakurugenzi. Huwezi kusajili kampuni ikiwa memorandum zako hazioneshi lolote kuhusu hilo.
Kimsingi nitaeleza machache japo yapo mengi kuhusu ukurugenzi na wakurugenzi katika kampuni. Kwa kampuni zetu ndogo ndogo za kijasiriamali mara zote wakurugenzi ndio hao hao wamiliki na ndio hao hao wana hisa. Niseme mapema tu kuwa si kosa kuwa hivyo isipokuwa yatupasa kufahamu kuwa kuna tofauti kati ya wakurugenzi, wanahisa, na wamiliki.
Wakurugenzi wanaweza kuwa watu wa kuajiriwa na wasiwe na uhusiano wowote katika umiliki. Unakuta mtu ameajiriwa tu kama mkurugenzi kwa ajili ya kuendesha kampuni pengine kutokana na elimu yake, uwezo wake, uzoefu n.k. Mwanahisa naye anaweza kuwa mwanahisa tu na asiwe mkurugenzi na mmiliki anaweza kuwa mmiliki tu na asiwe mkurugenzi. Isipokuwa tu mmiliki lazima awe mwanahisa kwasababu hakuna namna ya kufikia kuwa mmiliki wa kampuni bila kuwa mwanahisa.
Hivi ni vitu ambavyo huwezi kuvitenganisha. Mara nyingi wanaotenganisha umiliki, ukurugenzi na uanahisa ni wenye makampuni makubwa. Makampuni yetu madogo ya kufuga kuku mkurugenzi ndiye mmiliki na ndiye mwanahisa. Tutaona baadhi ya mambo hapa chini kuhusu ukurugenzi wa kampuni.
1.NINI MAANA YA MKURUGENZI.
Sheria ya Makampuni tunayotumia hapa nchini imetoa tafsiri nyepesi ya maana ya mkurugenzi kwa kusema kuwa mkurugenzi ni mtu yeyote ambaye amepewa nafasi ya ukurugenzi. Sheria hiyo inasema hivyo kwa kumaanisha kuwa ili umwite mtu mkurugenzi au hapana itategemea na na majukumu anayotekeleza katika kampuni. Ni majukumu tu ndio yatamtambulisha mtu kama mkurugenzi.
Hii ina maana yawezekana mtu akawa anaitwa mkurugenzi lakini hana majukumu ya kiukurugenzi. Kwa tafsiri hii huyu kisheria sio mkurugenzi. Mwingine yaweza kuwa anaitwa mwenyekiti lakini akitekeleza majukumu ya kiukurugenzi. Huyu kisheria atatambulika kama mkurugenzi. Kwa hiyo kwa kujibu wa tafsiri hii kumbe tunaona kuwa ukurugenzi ni majukumu wala sio jina.
Pamoja na hayo baadhi ya Mahakama huko Wingereza zimekuwa zikitoa tafsiri mbalimbali kuhusu maana ya ukurugenzi ambapo tafsiri iliyokubalika sana ni ile inayosema kuwa mkurugenzi ni mtu ambaye ana mamlaka ya kimwongozo, kimaadili na kiutawala katika shughuli zote na za kila siku za kampuni.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...