Asasi zisizo za kiserikali zinazojishughulisha na shughuli za Kilimo biashara za masharika ya TAHA, SNV,MVIWATA, AGRO PRO FOCUS,HIVOS, TCCIA na TRIAS leo zimefanikisha kufanya maonesho ya Kuunganisha Wakulima na Fursa za Mikopo ambayo yamelenga kuwakutanisha wakulima na wafanya biashara wa mazao ya kilimo pamoja na Taasisi za kifedha na zile zinazotoa mikopo kwa ajili ya shughuli za Kilimo Biashara. Katika picha ni Eneo la viwanja vya Kwaraa Halmashauri ya Wilaya ya Babati ambavyo vinatumika kwa ajili ya kuwakutanisha wakulima na taasisi za kifedha zinazotoa mikopo kwa wakulima(Habari Picha na Pamela Mollel wa jamiiblog)
Afisa wa NMB akifafanua jambo kwa mkulima wakati wa maonesho hayo yaliyofanyika Katika Halmashauri ya Wilaya ya Babati kwenye Viwanja vya Kwaraa na yamefunguliwa na Mwenyekiti wa chemba ya biashara Mkoa wa Manyara ndugu Athumani Karunde.
Kulia Mkurugenzi wa TAHA Bi. Jacqueline Mkindi akiwa na Mgeni rasmi ndugu Athumani Karunde wakati wa kutembelea mabanda ya waoneshaji
Wakulima wakipokea maelezo ya namna ya kuunganishwa na fursa za Mikopo toka kwa maafisa wa TAHA.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...