IMG_7697
Mkurugenzi wa kupunguza umaskini kutoka Wizara ya Fedha, Ana Mwasha (kulia) akifungua kongamano, linalojadili yaliyojiri katika Malengo ya Millenia na nini kinastahili kufanywa katika SDG's ili kuhakikisha mafanikio katika ukumbi wa mikutano wa Taasisi ya Uchumi na Utafiti wa Kijamii nchini (ESRF). Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Uchumi na Utafiti wa Kijamii nchini (ESRF) Dk.Oswald Mashindano na Katikati ni Naibu Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP)- Programme, Amon Manyama.(Picha na Zainul Mzige wa modewjiblog)

Na Mwandishi Wetu
MKURUGENZI wa Kupunguza Umasikini kutoka Wizara ya Fedha, Anna Mwasha amesema changamoto za uwezo wa kifedha kutekeleza miradi mbalimbali iliyokuwa katika Malengo ya Milennia, zinatoa ishara tosha ya kubadili mikakati ili kuwa na mafanikio katika Mipango ijayo ya Maendeleo Endelevu (SDGs).

Alitoa kauli hiyo jana wakati akizungumza na washiriki wa kongamano, linalojadili yaliyojiri katika Malengo ya Millenia na nini kinastahili kufanywa katika SDGs ili kuhakikisha mafanikio.

Alisema ipo haja ya kuimarisha makusanyo ya fedha za ndani na kuacha kutegemea wahisani, kwa kuwa moja ya sababu za kushindwa kutekelezwa kwa Malengo ya Millenia ni ahadi za wahisani kutotekelezwa.

Alisema kipengele cha nane katika Malengo ya Millennia, kiligusia ushirikiano wa kimataifa, ahadi ambazo amesema ukiachia nchi za Luxemburg, Denmark, Sweden na Norway, mataifa mengi hayakutoa asilimia 0.7 ya pato lao la ndani, ambalo lilikubalika kimataifa kusaidia Malengo ya Millennia kwa nchi masikini.

Alisema ili kuwepo na mafanikio katika miradi mipya na ile inayoendelezwa kutoka MDGs, iko haja ya kuangalia jamii iliyopo vijijini, ambako ndiko kwenye umasikini wa kutisha, ingawa Tanzania imefanya vyema kuondokana na umasikini wa chakula.

Umasikini wa chakula umepungua hadi asilimia 9 wakati Malengo ya Millenia yalikuwa ni asilimia 11.
Alisema ipo haja ya kufungua mawasiliano ya vijijini, kuinua kilimo, kuwapatia nafasi ya masoko na kuinua huduma za jamii.

Pamoja na kuzungumzia uwezo wa kifedha, alisisitiza haja ya wadau kuangalia namna ya kushirikisha sekta binafsi katika kutafuta vyanzo vya fedha kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ili kukabili umasikini.
IMG_7692
Naibu Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP)- Programme, Amon Manyama akizungumza kwenye kongamano la siku moja linalojadili yaliyojiri katika Malengo ya Millenia na nini kinastahili kufanywa katika SDG's ili kuhakikisha mafanikio lililofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Taasisi ya Uchumi na Utafiti wa Kijamii nchini (ESRF).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...