Mashindano ya kombe la Muungano Mufindi yaliyofunguliwa na Naibu Waziri Mhe. Juma Nkamia, tarehe 10 mwezi huu katika uwanja wa shule ya msingi lgowole, Mufindi, yanaendelea vyema.
Kwa mujibu wa mratibu wa michuano hiyo, Daud Yassin. Mashindano hayo yatakamilika tarehe 7 mwezi juni. Yassin kwa sasa anajitahidi kutafuta wahisani wa kuchangia zawadi za washindi, ambapo bingwa atapata cash ya shilingi milioni 5, mshindi wa pili 2.5m na mchezaji bora laki 5.
Yassin amewaomba wadau wa michezo, hasa viongozi, wachangie pesa hizo iIi michuano hiyo itakapo kamilika zawadi ziwepo.
Alisema amekubaliana na wenzake kwamba mwaka huu ni wa mwisho kwake kuratibu mashindano hayo.
Alianza kuratibu tangu mwaka 1996 hadi sasa.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo Mhe Juma Nkamia akisalimiana na wachezaji wa timu ya Mbeya City wakati wa ufunguzi wa michuano ya kombe la Muungano Mufindi, mkoani Iringa
Mhe. Nkamia akisalimiana na wachezaji wa lgowole fc
Mhe. Nkamia akipiga mpira kufungua rasmi mashindano hayo
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...